@king.media93: Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi. Mojawapo ya tawala ilikuwa ni dola ya wachagga (Chagga state). Dola hiii ilikuwa na Kiongozi Mmoja aliyeitwa Mangi Mkuu Mangi mkuu aliteua Mamangi wadogo wadogo (RC, DC) mfano Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc. January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu, Petro Marealle, John Maruma na Thomas Marealle. Thomas Marealle aliibuka Mshindi katika Uchaguzi huo Turudi nyuma Kidogo, mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya). Huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa miaka hiyo hadi sasa ndio Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro. Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya. Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasi ya maendeleo. Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo. Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University. Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe, Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala. Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka 1884/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state' iliyogawanywa. Shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru kutokana na umahiri wake katika uongozi lakini Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabila mengine nje ya wachagga. Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake. Nyerere alisema ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine. Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza. Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.

KING 🤴 MEDIA
KING 🤴 MEDIA
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 06 July 2026 21:33:54 GMT
62831
1623
77
194

Music

Download

Comments

julius.ndalu6
KIJANA WA YESU🕊️ :
Hao jamaa wangekuwa mbali sana kiuchumi.
2026-07-08 09:15:44
55
nervousgirl2026
Empress 👑 :
Mm mjukuu wa mangi Sina ,Babu yangu Mungu ampumzishe Kwa aman
2026-07-08 10:12:58
22
jolly...m4
💦Jolly⚘️💦🌹 :
🥰🥰🥰proud to be 🙌🙌🫡
2026-07-09 07:27:32
1
smile_for_me.999
Daudi :
Chagga for life
2026-07-08 15:27:40
18
bintimosha24
@bintimosha24 :
wangetuacha tuu na nchii yetu wallah 🥰😭😭😭😭
2026-07-08 19:37:27
16
_herself6
Daddy’s girl❤️ :
I am proud of my tribe❤️wallah
2026-07-08 19:48:51
5
stella.shiyo
mashio og👌 :
tungkuwa mbali sana 🥰
2026-07-08 19:29:01
1
user5667391774330
user5667391774330 :
daah
2026-07-09 07:36:07
0
swahib876
young swaah :
au sio
2026-07-07 05:07:30
4
mimaaxly
mimaaxly :
alitukosea sana
2026-07-08 11:19:47
7
beatricemushi867
Beatrice Mushi867 :
wangetuacha tu 🥰🥰🥰
2026-07-08 18:50:25
3
firospatial
GIS and Remote sensing life🌍 :
babu pumzika Kwa amani🙏
2026-07-08 11:55:23
6
iamchagga
iamchagga :
Angetuacha tu leo tungekuwa mbali sana kiuchumi
2026-07-09 06:18:43
0
glorysandy1
Ms _ Sandy ♋️ 💧 🌕 :
Alituponza
2026-07-09 05:39:01
0
gee62995
Gee :
Tungekua mbali sana kiuchumi
2026-07-08 20:43:04
0
ma.mish2
ma mish 🎂 :
najivunia kabila langu😁🥰
2026-07-08 19:37:52
0
user526199866172
user526199866172 :
babu kubwa sana
2026-07-08 08:25:27
0
user3cd4jleobf
Nellywise :
One days yes. Ideas is stilling there
2026-07-08 20:23:01
1
user62672395902807
Doreen :
Ingekuwa poa sana jaman
2026-07-09 05:33:58
0
user0621889732
issa mbisa :
aman iwe nawe milele
2026-07-08 18:48:23
0
user6154713795456
happy :
ingekuwa hivyo ingependeza sana
2026-07-08 19:07:27
0
carenjohn895
SWET_AFRICA🙏 :
kannchi ketu kangekua kama ulaya walahi🥰🥰
2026-07-08 09:41:34
11
mohamedwaziri8
Mo Waziri :
Wangekuwa mbali sana kwa sababu wachaga wana akili
2026-07-07 06:24:09
31
george.shirima1
George Shirima :
1952,Tayari Anayo Masters Degree🎓,M16 Wanamkubali Na Wanapendekeza Awe President,Amepata Elimu Yake Ndani Ya Chuo Bora Cambridge University Miaka Hiyo,Dola Yenye Mamlaka Kamili,Askari Wazuri Wenye Mafunzo Smart,HILA KWA KUA ALIKUA "supreme Cognitive",Alikabidhi Kwa MWL.🤝
2026-07-07 14:11:06
10
ahmedsalmiy83
Ahmed Al salmiy :
wabaguzi sana
2026-07-08 02:07:11
0
To see more videos from user @king.media93, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About