@abdul.machine8: UJUMBE WANGU KWA JAMII Mimi ni Mwenyekiti wa Sauti Para Sports Club, lakini zaidi ya cheo hicho, mimi ni mtumishi wa ndoto za wachezaji wetu. Kwa sababu klabu yetu bado haina mfadhili wa kudumu, nimeamua kubeba majukumu mbalimbali ili kuhakikisha timu inaendelea kusimama. Mimi ni Mwenyekiti, Kocha Mkuu, mtengenezaji wa magongo ya wachezaji, mpiga picha wa timu, mwandishi wa barua na nyaraka za klabu, msimamizi wa mitandao ya kijamii, na hata ninagharamia baadhi ya mahitaji kama bando la mawasiliano. Sikuchagua kuwa kocha kwa sababu nilikuwa natafuta nafasi hiyo, bali nililazimika kubadilisha changamoto kuwa fursa. Kila kocha tuliyemleta aliondoka kutokana na kukosekana kwa malipo. Badala ya kukata tamaa, niliamua kujifunza, kusoma kozi za ukocha na kujiendeleza ili niweze kuwapa wachezaji wetu mafunzo bora. Ninaamini uongozi wa kweli si kusubiri wengine wafanye, bali ni kuanza na kile ulicho nacho kwa ajili ya watu unaowaongoza. Sauti Para Sports Club ni zaidi ya timu; ni familia, ni tumaini na ni jukwaa la kuonyesha uwezo wa watu wenye ulemavu kupitia michezo. Naendelea kujitolea kwa moyo wangu wote, nikiamini siku moja juhudi hizi zitazaa matunda na ndoto za wachezaji wetu zitatimia. Nakushukuru sana @Boston Kalata kwa video hii. @chezafoundation @MguuUtaongea

Abdul Machine
Abdul Machine
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 07 July 2026 09:26:43 GMT
395
19
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @abdul.machine8, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About