@stuadventist: Jumatano ya Maombi Ipo nguvu katika maombi. Tunapomrudia Mungu kwa moyo wa unyenyekevu, hatusimami peke yetu Yeye hutusikia, hutujibu kwa wakati wake, na hututia nguvu za kuendelea. Haijalishi unapitia nini leo, usikate tamaa. Piga magoti, fungua moyo wako mbele za Mungu, kwa maana hakuna ombi la imani linalopotea mbele Zake. Mungu bado anasikia. Mungu bado anajibu. Mungu bado anatenda. Karibu tuungane katika maombi na tumkabidhi Bwana kila hitaji letu.