@mpamb4naji: Hakuna mtu mkubwa kuliko kazi yake. Siku ukianza kuona kazi za msingi ni ndogo kwako, ukadharau majukumu yanayojenga matokeo, na ukajiona umevuka kiwango cha kufanya kazi yako vizuri—ujue nafasi yako inaanza kuwa hatarini. Kila kazi ina mtu anaweza kuifanya. Ukiacha kuleta thamani, nidhamu na uwajibikaji, atakuja mwingine akafanya, na pengo lako lisionekane. Usijione mkubwa kuliko kazi; ifanye kazi yako kwa kiwango ambacho ni vigumu kubadilishwa. #Kazi #Nidhamu #Uwajibikaji #Mafanikio #Biashara