@amrisali_ifx: Last month nilipata msiba wa mama yangu mkubwa (Rest in peace) nikasafiri kuelekea Mwanga, Wakati nipo njiani alinipigia rafiki yangu wa muda mrefu jina sitamtaja japo amekubali niandike ujumbe huu hapa, Alikuwa anataka tuonane ana issue very sensitive ambayo asingeweza kuniambia kwa simu, kumuambia nimesafiri alikuwa tayari hata kutoka Dar kunifata Kilimanjaro, long story short nimerudi Dar tu kesho yake tukakutana, unadhani alichokuwa anataka ni nini? Kujifunza forex trading, cha kwanza kumuuliza ni “mbona ghafla?” Hapo ndo akaanza kunipa mkasa wa yaliyotokea kazini mpaka kufikia kufukuzwa kazi yeye na wafanyakazi wenzake 7, alikuwa anakunja around 3M kwa mshahara na pesa nyingine anazopata nje ya mfumo, hii kazi ilikuwa ni kila kitu kwenye maisha yake, Nikamueleza tu ukweli kwamba forex sio sehemu ya kukimbilia baada ya kupoteza kazi na hawezi kufanya replacement ya mshahara kwa kutumia Fx kwa haraka kama anavyodhani, japo kiroho ngumu ilitakiwa nimuulize tu “siku zote ulikuwa wapi?,” ila nikaona sio wakati sahihi, Nilimuelezea sana kwanini hii sio option sahihi kwake kwa sasa, Siku nne tu mbele kanicheki tena anasema ana bonge moja la business idea anataka niwekeze tushirikiane, akanielezea sana hiyo idea ilibidi nimuambie tena ukweli kwamba, “Hiyo idea sidhani kama ni practical ila pressure ndio zinafanya uone ni brilliant idea, na nipo tayari kukuchangia mtaji ila ikiwa ni idea iliyonyooka, Kitu nataka kusema kwa kila mtu hapa ni; Usisubiri maisha yakuweke kona mbaya ndipo uanze kufanya maamuzi muhimu; - Usisubiri uingie kwenye crisis ndipo uanze kutafuta mentors, ushauri, partnership au mtaji, - Usisubiri ubaki na pesa zako za mwisho ndipo uanze kujifunza kuwekeza, - Usisubiri uumwe ndipo uanze kula vizuri na kufanya mazoezi, - Usisubiri upoteze ajira ndipo uanze kujifunza ujuzi au kuanzisha biashara, - Usisubiri uwe na majanga ndio upigie watu simu, - ⁠Usisubiri biashara yako iingie matatizoni ndio ufungue biashara nyingine, Hakuna kitu kibaya kama kuacha kufanya maamuzi mpaka siku uwe kwenye pressure au mpaka maisha yakunyime options,

Amrisaly IFX
Amrisaly IFX
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 08 July 2026 15:36:23 GMT
22262
1162
19
23

Music

Download

Comments

olespano
Michael Julius756 :
On point bro🔥🫡
2026-07-09 08:38:26
0
masterfunyo
Masterfunyo :
exactly🤝
2026-07-08 19:21:38
2
maningehtrends
MANINGEH TRENDS :
Big fact my bro
2026-07-08 15:58:11
2
hipolitimushi
hipoliti :
I think many books can be written from your message.....short but deep meaningful
2026-07-08 21:08:38
2
emmaseba
emmaseba :
2026-07-09 07:29:15
0
gemy_tz_wakala
GEMY TZ :
100%
2026-07-09 06:04:04
0
777.com296
@uchumifresh.com :
pole sana
2026-07-09 07:22:16
0
mark002266
mark002266 :
bro nikiwa mkubwa nataka kuwa kama ww
2026-07-08 16:30:35
0
samwelsamgo6
SamGO :
Tangu nimeanza kukufatilia bro, kuna vitu vingi najifunza
2026-07-08 17:09:03
0
iam_baraka93
iam_baraka93 :
Pole san
2026-07-08 16:32:21
0
hamidumkwizu05
ENGINEER PUYOL🦈 :
Tulikuwa wote msiba mwanga kak mungu mmalaze mahar pema pepon😔
2026-07-09 04:36:48
1
rebeccandoto
Rebecca :
hata mm nataka kujifunza... na ninasababu natamani niiseme ila ni ndefu kidogo
2026-07-09 08:44:17
0
transport_contentcreator
Mr_Logistics✈️ :
Somo kubwa
2026-07-08 21:10:31
0
itsmystic_pulse
mysticpulse.x :
💪💪💪
2026-07-08 16:00:26
1
letslive_777
𝐌𝐚𝐫𝐢𝐚 :
📌
2026-07-08 22:11:53
0
tinyjr26
Tiny Jr :
✊🏽
2026-07-08 19:57:39
0
buzingoone_marketing
buzingoone_marketing :
🙏🏻
2026-07-09 08:36:47
0
irenekimbori
Angela kimbori :
🥰🥰🥰
2026-07-09 08:59:39
0
To see more videos from user @amrisali_ifx, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About