@brainplus0091: حَسْبِيَ اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ Hasbiyallāhu lā ilāha illā Huwa, ʿalayhi tawakkaltu, wa Huwa Rabbul-ʿArshil-ʿAẓīm. "Mwenyezi Mungu ananitosha. Hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Kwake nimeweka tawakkul yangu, naye ndiye Mola wa Arshi Tukufu." Hii ni sehemu ya Quran, Surah At-Tawbah (9:129). Pia imepokelewa katika hadithi kwamba mwenye kusema dhikri hii mara saba asubuhi na jioni, Mwenyezi Mungu humtosheleza yale yanayomhangaisha. Wanazuoni wametofautiana kuhusu nguvu ya riwaya hiyo, lakini maneno ya aya yenyewe ni ya Qur'ani na ni dhikri nzuri ya kumtegemea Mwenyezi Mungu.