@yoniproduct_255: Ovulation strip ni kifaa kinachotumika kupima ongezeko la homoni ya LH (Luteinizing Hormone) ambayo huongezeka kabla ya ovulation (yai kutoka kwenye ovari). Faida za kutumia ovulation strip: ✅ Husaidia kujua siku zako zenye uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito. ✅ Huonyesha muda wa ovulation kwa usahihi zaidi kuliko kuhesabu siku pekee. ✅ Husaidia kupanga tendo la ndoa katika siku zenye nafasi kubwa ya mimba. ✅ Ni rahisi kutumia ukiwa nyumbani na matokeo hupatikana ndani ya dakika chache. ✅ Hufaa kwa wanawake wenye mizunguko isiyo sawa sawa ya hedhi ambao hupata ugumu kujua siku za rutuba. ✅ Husaidia kupunguza kubahatisha kuhusu siku za ovulation. Jinsi ya kutafsiri matokeo: * Mistari miwili na mstari wa test ni mweusi sawa au zaidi ya control = LH surge imeonekana; ovulation inaweza kutokea ndani ya saa 12–36 zijazo. * Mstari wa test ni hafifu kuliko control = bado hujafikia LH surge. * Mstari mmoja tu wa control = matokeo ni negative. Kwa anayelenga kupata ujauzito, inashauriwa kufanya tendo la ndoa siku ambayo strip imeonyesha positive na siku 1–2 zinazofuata.