@salmamrisho1: Mamlaka husika zimeanza uchunguzi kubaini chanzo cha moto ulioharibu sehemu ya Kituo cha Mafuta cha Lake Energies kilichopo Kata ya Bombambili, Manispaa ya Geita, huku ikithibitishwa kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo. Moto huo ulizuka wakati gari aina ya Kenta lenye namba za usajili T 799 BEB, mali ya Abdul Rajabu, likiwa linajaza mafuta katika kituo hicho. Kwa mujibu wa taarifa za awali, moto ulianzia kwenye gari hilo kabla ya kusambaa na kuharibu sehemu ya miundombinu ya kituo. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Keneth Mwakasitu, amesema kikosi cha zimamoto kimefanikiwa kuudhibiti moto huo kabla haujasambaa kwenye maeneo mengine. Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo halisi cha moto huo. Kwa upande wake, mmiliki wa gari hilo, Abdul Rajabu, amesema alishuhudia moshi ukitoka kwenye sehemu ya bodi ya gari wakati likiwa linaendelea kujaza mafuta, kabla ya moto kuzuka, akieleza kuwa hafahamu chanzo cha tukio hilo.

Salma Mrisho
Salma Mrisho
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 10 July 2026 13:53:47 GMT
32146
663
6
40

Music

Download

Comments

user8852279269090
Emanuely 💯💯 :
poleni
2026-07-10 20:01:52
1
yassinmohamed1346
yassin555 :
pole sana brother BAYA..
2026-07-10 20:37:15
0
kilomoclain
amos clain :
saf kabisa
2026-07-10 19:12:57
0
boundaryfire
boundary fire :
poleni sana
2026-07-10 17:30:28
1
janepher.jacob
Janepher Jacob :
du
2026-07-10 20:27:00
0
chimwe840
chimwe :
kwahiyo gari lililokuwa limebeb tenk za mafuta lilikuwa halijazimwa kwahiyo umeme wa betri haukiwa sawa
2026-07-10 15:39:45
1
To see more videos from user @salmamrisho1, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About