@mshauri_kazini: ⚖️ Kusitisha ajira si uamuzi wa hiari wa mwajiri. Kwa mujibu wa sheria za kazi za Tanzania, kusitisha ajira kunapaswa kuzingatia mambo mawili muhimu: ✅ Fair Reason – Lazima kuwe na sababu halali na ya haki ya kusitisha ajira. ✅ Fair Procedure – Lazima mwajiri afuate utaratibu wa haki, ikiwemo kumjulisha mfanyakazi tuhuma au sababu, kumpa nafasi ya kujitetea, na kufanya uamuzi kwa kuzingatia sheria na kanuni husika. Ukikosekana hata kimoja kati ya hivyo, kusitisha ajira kunaweza kutafsiriwa kuwa unfair termination na mwajiri anaweza kuwajibika kisheria. 📚 Fahamu haki zako, zingatia wajibu wako.#kazinikazi👊👊 #elimu #fyp #tiktoktanzania🇹🇿 #sheria