@chawamata_tv: VIDEO: Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Madogo na ya Kati Tanzania (TAMSTOA), Chuki Shabani, amesema chama hicho hakitanyamaza kufuatia tukio la mmiliki wa lori ambaye pia ni dereva, Khalfan Ndamo, kudai kushambuliwa na kuporwa akiwa ndani ya ICD ya Farion, Sabasaba, wilayani Temeke. Akizungumza kuhusu tukio hilo, Shabani alisema taarifa za awali alizipata kupitia kundi la Usalama Kwanza la sekta ya usafirishaji, ambapo ilielezwa kuwa Ndamo alikuwa amepelekwa kushusha kontena lakini akaambiwa makontena hayo hayangepokelewa kutokana na wenye mizigo kuchelewa kuyachukua. Alisema dereva huyo alijaribu kuomba maelekezo ya mahali pengine pa kushusha kontena kwa kuwa hakuwa na sehemu nyingine ya kuegesha lori, lakini badala yake alidai kushambuliwa na watu walioitwa kwenye eneo hilo. Mwenyekiti huyo alisema mara baada ya kuona video ya tukio hilo aliwasiliana na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi zinazohusika ili hatua zichukuliwe haraka. Alisema tayari ametuma taarifa pamoja na vielelezo kwa Mkurugenzi wa TASAC, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), pamoja na Kamati ya Tanzania Ports Improvement Committee ili mamlaka hizo zipate kufahamu kinachoendelea katika baadhi ya ICD binafsi. Kwa mujibu wa Shabani, Mkurugenzi wa TASAC tayari amemjibu kuwa suala hilo linafanyiwa kazi kwa haraka, huku akisema anatarajia kuanza kukutana ana kwa ana na viongozi wa taasisi mbalimbali kuanzia Jumatatu ili kufuatilia hatua zinazochukuliwa. Shabani alisisitiza kuwa TAMSTOA itatoa msaada wa kisheria kwa mwanachama wake na kuhakikisha suala hilo linafikishwa mahakamani endapo uchunguzi utabaini kuwepo kwa makosa ya jinai. Aidha, ametoa wito kwa mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mazingira ya usalama katika vituo vya kuhifadhi makontena (ICD) ili kuzuia matukio ya aina hiyo kujirudia na kuhakikisha madereva na wamiliki wa malori wanatekeleza shughuli zao katika mazingira salama. FULL VIDEO IPO YOUTUBE YA CHAWAMATA TV. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #madeintanzania #SupportLocal #madeintanzaniat #roadto100followersontwitch #madeintanzaniawith #madeintanzania🇹🇿 #viraltz
CHAWAMATA TV
Region: TZ
Saturday 11 July 2026 08:21:47 GMT
Music
Download
Comments
Roby Roby :
asanteeh
2026-07-11 16:00:31
0
fundi idi :
safi kabsa
2026-07-11 12:11:14
5
@mr introvert 🎶 :
mzee wa maana kabisa 👏👏👏
2026-07-12 07:23:22
2
deo rutha :
hongera sana mkuuu
2026-07-11 21:11:14
4
TRIPLE L :
Mungu ana kazi nyingi za kufanya kwa hili msimwachie Mungu msaidieni maana lina wezekana kulipambanoa
2026-07-12 05:31:32
1
kandolomnyamwezi :
kuomba radhi hakusaidii
2026-07-12 09:34:16
1
benny haule :
nakubali kiongoz
2026-07-11 14:59:12
2
user6023109638541 :
safi sana mzeee
2026-07-11 11:06:00
4
Doreen Willbard :
asante baba
2026-07-11 11:59:51
4
AllahumaAmeen :
nice
2026-07-11 11:30:46
1
anord :
ongela mzeewetu
2026-07-12 12:47:24
1
V-@Wambura :
safi sana mzee
2026-07-11 10:29:59
4
BABA BRIAN :
tusaidie tuu baba mkubwa mungu atakulipa mema. hii umungu mtu sio haki chini ya hili jua
2026-07-11 13:35:40
2
BAMBA.xtwo🦺🇹🇿 :
saf kabisa
2026-07-11 10:56:14
1
user5961350943797 :
safiiiii
2026-07-11 20:23:34
1
mosescheyo2023 :
Safi sana mzee wangu unapambana sana nakumbuka mwaka jana Victoria tazara ulinisaidia sana mungu akuweke 🙏
2026-07-11 22:58:35
0
Whichseed :
safi
2026-07-11 14:58:53
0
👑 KiBELLa oG :
ila vyama vingi sana aise
2026-07-11 23:12:06
0
The Blessed 😇 John. :
Excellent
2026-07-11 18:29:02
0
M TZ halisi :
safi sana baba
2026-07-12 23:14:11
0
Alufani Lombwe :
Safi Sana kiongozi
2026-07-11 10:05:31
0
Idrissa Jumbe :
Hii ndio inaleta maana ya umoja wenu,na sio kuomba radhi tu wakati kamjeruhi mtu amlipe na fidia.
2026-07-11 10:01:02
1
Tumaini :
😭😭😭 daaaah inaumiza
2026-07-11 13:26:36
0
TATA BM🦅🇹🇿(NYEBHOSA) :
SASA SISI KAMA WAUMIN MIMI NI MKRISTO ILA HILI NIMEPENDA MUNGU AKULINDE SHEIKH
2026-07-12 17:52:14
0
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm
homepage.