@tanzaniaembassyinoman: Jana nilifanya mazungumzo muhimu na Mawakala wa Ajira nchini Oman wanaoratibu ujio wa wadada wa kazi za nyumbani—ambalo ndilo kundi kubwa la Watanzania waliopo hapa. Tulijadili kwa uwazi changamoto na wajibu wa wafanyakazi, mawakala, na waajiri. Mambo makuu tuliyokubaliana: 1️⃣ Mikataba na Ulinzi wa Kisheria: Ubalozi utaongeza mikataba ya nyongeza ili kulinda haki za mwajiri na mwajiriwa. Itaainisha wazi kima cha chini cha mshahara, bima ya afya, muda wa kazi/mapumziko, likizo, kiinua mgongo (gratuity), na tiketi ya kurudi nyumbani. Tulisisitiza mikataba hii iheshimiwe na kuwepo kwa uwajibikaji wa kisheria kwa pande zote. 2️⃣ Maandalizi Kabla ya Safari: Kuandaa wadada wetu kabla ya kusafiri ili wajue mila, desturi, mazingira ya kazi ya Oman, na matumizi ya vitendea kazi vya kisasa. 3️⃣ Kikao Kazi cha Pamoja: Kufanya kikao kikubwa kitakachojumuisha Mawakala, Ubalozi, pamoja na Wizara na Taasisi za Serikali za Tanzania na Oman zinazosimamia masuala ya Ajira. Lengo ni kukomesha unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya waajiri, kudhibiti utovu wa adabu au uvunjifu wa sheria kwa baadhi ya wasichana, pamoja na kuwashughulikia maajenti wasio waaminifu. Lengo letu kuu ni kutokomeza usafirishaji haramu wa binadamu, kulinda taswira ya nchi yetu, na kuimarisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Oman. Ubalozi utashukuru kupata maoni yenu ya ziada; je, ni nini zaidi kifanyike ili kuhakikisha tija na ufanisi kwenye jambo hili? Toa maoni yako hapa chini 👇🏾
Tanzania Embassy In Oman
Region: OM
Saturday 11 July 2026 11:51:55 GMT
Music
Download
Comments
schön :
Hello to my Embassy Oman next meeting I want to join you to represent my colleagues thank you so much 🇹🇿
2026-07-12 06:17:04
3
Moohad1 :
Wish I could join
2026-07-12 05:12:25
1
esma melanin🇹🇿🇴🇲♋ :
atuna ijaza jaman tunachoka akili mpka mwili 😭
2026-07-11 18:36:43
82
Scolastica Mbamange :
Kwanini mikataba inaandikwa rial 120 lakini tunapewa rial 80 au 90.?
2026-07-12 10:30:12
5
Isham✨ :
Asalam Aleykum Hii ishu za nyie kubadilisha sijui kusimamia mambo yaende sawa me naona kam mnafanya kwa ajili ya kutupa moyo walahi watu wanatekeni sana na kuna wengine wako sawa ila me naongea kwa niaba ya wengine me siko vibaya hamdllah ila kuongea hapo haitoshi inatakiwa muajiriwa na muajiri wakalishwe kwanza pamoja na kila mtu aambiwe haki zake mbele ya ofisi ku aliyofikia na kam ikiwa tofauti mtu awe na uhakika wa kupata msaada ndio maan watu wanatoroka miak mingi tunaskkia tu kimebadilishwa hichi lakin kwa kusikia sio kwann vitend tunakula kwa moyo wetu ila pia tunaipa nchi yetu kipato Allah anaona so kuweni wema sie binadam jmn oneni kam watt wenu maan hamn aliechipuka kweny mti asanten na samahnini kam nimeongea mahali vibay Allah awafanyie wepesi 🙏🙏🌹
2026-07-11 18:23:14
55
Noor Abdul :
mshahara ndio kila kitu upande 150 kwa kila 🥺🥺
2026-07-12 00:14:31
13
1996Maria Samson :
mishahara midogo hailingani na kazi tunazo fanya pia tunafanyishwa kazi kwenye nyumba mbili hata ijaza hatupati wengine. mtusaidie jamani
2026-07-11 19:00:33
12
الشفاء 💚 :
nime muona agent wang Salma Abdullah Al hasbi🥰
2026-07-11 20:48:48
9
WARDA 93🇹🇿 :
mashallah ila msitusahau na mashagara.oman
2026-07-11 17:18:23
8
Bethleo :
kuna nini mbona mie sina taarifa😅
2026-07-11 18:09:27
5
Salma💕 :
kaka khalfani Allah azidi kukupa umri mrefu🥰🥰
2026-07-11 17:36:03
10
MSUKUMA MPOLE😇TZ🇹🇿👉🇴🇲 :
Kwali waongeze mishahala maana kazi nyingi hawataki tupumzike jamani au kwangt
2026-07-11 19:39:05
13
@pretty dee :
msisahau jaman maximum ya mshahara jaman sisi pia ni nguvu kazi ya taifa tunaumia sana kwenye mishahara
2026-07-11 18:43:34
20
Farima Fatima :
tunaomba mtusaidie tupate ljaza na mshahara tuongezewe maan kazi tunafanya nyingi muda wakupumzika hatuna mshahara midogo tukiumwa hatupumziki Wala kwenda hospital
2026-07-12 06:12:29
7
Salma Mohamed :
maskini mungu awalinde wadada wote mlioko huko
2026-07-12 08:53:40
3
Subira Ngaona :
jmn chonde chonde tunahitaji ijaza😭 wallah
2026-07-12 10:00:01
2
khadija Katonga :
mshahara jamani...tunapewa 80 tu...
2026-07-12 11:52:25
1
consolata :
kaka khalfani🥰🥰
2026-07-12 11:44:42
1
sasha 🥰 :
mwenye namba ya ubarozin naomba
2026-07-12 10:22:40
1
Haiba Adam :
Tunaomba Utusaidiye tupate mapumziko tunachoka sana kazi kila siku hakuna mapumziko na mishahara piya 🙏
2026-07-12 08:37:29
2
Umrath Pure 💖💝 Kirungi :
Hatuna mapumziko kuanzia january hadi desember kazi kazi hata ukiumwa unapewa panadol dakika 5 na uendelee na kazi
2026-07-12 09:08:16
4
dylan farida :
Mishahara midogo na ijaza atupati 🙏🙏
2026-07-12 06:41:48
3
Hassan Antony :
naomba no za ubalozi oman kuna tatizo naomba unisaidie
2026-07-12 08:39:28
3
user8766973586712 :
tuyasikie Haso mazungumzo sasa
2026-07-12 04:24:34
2
To see more videos from user @tanzaniaembassyinoman, please go to the Tikwm
homepage.