@ndoa.na.urithi: Wanawake wengi hujiuliza… “Kwa nini mume wangu hapendi kurudi nyumbani mapema?” Lakini hawajawahi kujiuliza… Anarudi nyumbani anakutana na nini? Anarudi kutoka kazini akiwa amechoka… Badala ya kupokelewa kwa utulivu… Anakutana na lawama. Anakutana na kelele. Anakutana na malalamiko. Anakutana na maneno ya kumkumbusha kila alichoshindwa kufanya. Hakuna hata dakika chache za kupumzika. Hakuna hata nafasi ya kuzungumza kwa utulivu. Matokeo yake… Kesho yake anaanza kujisemea: “Kwa nini nirudi mapema? Si nikichelewa kidogo ni yale yale.” Polepole… Nyumba inaanza kupoteza maana ya kuwa sehemu ya kupumzika. Inakuwa sehemu ambayo mtu anaingia kwa hofu. Mwanamke… Jifunze kuwa msaidizi wa mume wako. Usiwe sababu inayomfanya akimbie nyumbani. Kuwa sababu inayomfanya atamani kurudi mapema. Amani ya nyumbani haihitaji pesa nyingi. Inahitaji hekima, heshima na namna tunavyozungumza. Kumbuka… Nyumba yenye amani humfanya mwanaume atamani kurudi. Na mwanaume mwenye upendo na uwajibikaji humfanya mwanamke atamani kubaki. Ndoa haijengwi na mtu mmoja. Inajengwa na watu wawili. ✍🏽Ndoa na Urithi✅ #NdoaNaUrithi #Ndoa #Mahusiano #Mawasiliano