@miladu_tv: Baraza la BAKWATA limeazimia kuwasimamisha Masheikh wa Mikoa mitatu kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mienendo inayokiuka misingi ya kiuongozi ya Baraza hilo. Baraza hilo limekutana leo Julai 14, 2026 katika kikao cha dharura kilichoongozwa na Kaimu Mufti na Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ally Khamisi Ngeruko na kuazimia kuwasimamisha Masheikh hao. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hassan Said Chizenga, Masheikh waliosimamishwa ni Sheikh Walid Alhad Kawambwa wa Mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Issa Nassor Issa wa Mkoa wa Singida pamoja na Sheikh Hassan Kiburwa wa Mkoa wa Kigoma. Taarifa hiyo imeeleza kuwa utekelezaji wa maamuzi hayo unaanza rasmi leo Julai 14, 2026. Aidha, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Mbwana, amewateua Viongozi wa muda kushika nafasi hizo hadi pale hatua nyingine zitakapochukuliwa. Waliopewa nafasi hizo za Ukaimu ni Sheikh Abasi Ramadhani Abasi ambaye atakuwa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Issa Ramadhani Simba aliyeteuliwa kuwa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida na Sheikh Uwesu Mohamed Kiumbe ambaye atahudumu kama Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Kigoma. BAKWATA pia imeielekeza Ofisi ya Katibu Mkuu kusimamia makabidhiano ya ofisi hizo ndani ya muda mfupi. @miladu_tv #babdeoMiladu #MiladuUpdates

Babdeo Miladu
Babdeo Miladu
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 14 July 2026 13:44:55 GMT
53763
1958
159
236

Music

Download

Comments

user2345679887
mjbackup :
NACHOJUA MIMI NI KWAMBA SHEKHE WALID NI MOJA YA WANADAMU WAKIPEKEE SANA NA AMEBARIKIWA KUPENDWA NA NI KIONGOZI WA WATU HILI HALITABADILIKA KAMWE.ALLAH AMJAALIE MTU HUYU WA WATU KHERI NYINGI INSHAALLAH 🙏🏻
2026-07-14 15:19:04
52
madrasatu.alwahha
Madrasatu Al-wahhaab :
Unaweza ukalichukia jambo kumbe nikheri kwako. na unawaeza ukalipenda jambo kumbe nishari kwako. sikuzote sema Alhamdulillah
2026-07-14 14:50:20
25
prencerateo
prencerateo :
waislam wameumia sana
2026-07-14 15:07:26
34
yusufutuji223
yusuphutuji :
Allah atunusuru
2026-07-14 15:04:58
1
remmyshalismohamm
remmyshalismohamm :
itakua wamechunguza wakaona ni kweli kuhusu sheikh walid
2026-07-14 16:01:02
8
rwambo06
Rwambo :
weka sababu hapo
2026-07-14 16:05:16
3
dadamziwanda3
MAJINA MENGI 💫🫰 :
shekhe wardi mnamsimamisha kivipi mnauhakika na kinachoelendele kwenye mitandano duh 😭
2026-07-14 15:43:52
5
pilipili5082
pilipili :
jmn tuna mpenda shekh wetu plz
2026-07-14 16:08:51
0
meneja_suma1
MENEJA SUMA :
shekhe Walid mmemuonea sisi kama waislamu Bado tupo nae
2026-07-14 15:47:45
9
barkis_77
Golden saw :
hizo sababu mbona hamzitaji ss
2026-07-14 14:33:54
18
user6176312472429
user6176312472429 :
wasameheni jamani ,kutenda kosa sio kosa bali kuludia kosa ndio kosa,nawaombea msamaha muwasamehe jamani 😭
2026-07-14 16:02:23
1
rukhalrukhi
Rukhal Rukhi :
mungu ndo anajua ukweli zaid kama kuna khila yyote Allah ataibainisha mbele ya umma inshallah
2026-07-14 15:46:01
4
user43516822454057
Chanukah :
I'm proud to be Muslim
2026-07-14 15:36:53
0
mister.counsellor
mister counsellor :
mbona wamekimbilia kumsimamisha ghafla
2026-07-14 14:13:52
7
yasini.mbembati0
yasini mbembati :
Hakika huu ndio uislamu dini ya haki isiyofumbia macho uovu wowote
2026-07-14 16:04:41
4
mahibu_jr55
MAHIBU 55 👑🍀🍁 :
mungu akupe uvumilivu sheakh walid kpnz ch waisilamu
2026-07-14 16:36:40
1
user9298183661561
محمد بن صالح العثيمين :
hapo kuna Siri sheikh walidi aliashiriwa kupewa umufti nadhani muda umefika
2026-07-14 15:40:35
1
ismailomar6105
🔵 Ismail Care TZ ✔️ :
Hili lilisukwa ndo maana imekuwa harakaharaka ivyo kabla mambo hayajapoa😅
2026-07-14 16:25:55
1
chisokolelm
Chisokole LM :
Nimeumia sana, sheikh Walid, Allah akupe uvumilivu.
2026-07-14 16:24:32
1
aminaali2085
Amina Ali :
hila tu tunajuwa kama ni michezo mmefanya😭😭😭😭😭😭
2026-07-14 15:31:21
4
pokomo_vibes
𝐏𝐎𝐊𝐎𝐌𝐎 𝐕𝐈𝐁𝐄𝐒 🇰🇪 :
Sheikh Walid tunamhitaji ...bado hamja tupatia sababu ya kusimamishwa
2026-07-14 15:44:59
2
tashuu2018
DIDAH DIDAH :
Itakuwa ni funzo kwa ma sheikh wengine
2026-07-14 15:54:04
3
altiwany98
Altiwany :
tangu zamani nilisema hapo hakuna shekh
2026-07-14 15:21:50
3
kijana.wa.iran
Kijana wa Iran :
Walid ndo tunamtaka sisi
2026-07-14 15:54:18
0
mamsap47
mamsap :
ila jamani shekh wetu baadae atakuwa mufti inshallah ☺️
2026-07-14 14:56:55
4
To see more videos from user @miladu_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About