@badriya_attai: Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kijini, napenda kutoa shukrani zangu za dhati na za moyo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kutujengea Kiwanja cha Michezo cha Kijini chenye hadhi ya Mkoa. Mradi huu ni zawadi kubwa kwa vijana na wananchi wetu, kwani utafungua milango ya kuibua vipaji, kukuza michezo, kuimarisha afya, kuleta ajira na kuifanya Kijini kuwa kitovu cha mashindano na maendeleo ya michezo. Tunathamini sana uwekezaji huu wa kihistoria na tunaahidi kukitunza kiwanja hiki ili kiendelee kuwa fahari ya Kijini na Zanzibar kwa ujumla kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

badriya_Attai
badriya_Attai
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 14 July 2026 16:56:01 GMT
177
16
1
1

Music

Download

Comments

awenaammar
aunty_awena :
mashaallah🥰🥰🥰
2026-07-14 18:21:00
0
To see more videos from user @badriya_attai, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About