@daxbreeezy: Ripoti ya hivi karibuni kutoka HypeAuditor ya tarehe 8 Julai 2026, inaonyesha akaunti ya mchezaji kandanda maarufu duniani Cristiano Ronaldo ya Instagram ina takriban wafuasi milioni 674.Jambo hilo linamfanya aendelee kusalia kuwa mtu anayefuatiliwa zaidi ulimwenguni kwenye mtandao huo.Makadirio ya idadi ya watu duniani ya mwaka 2026 kutoka mtandao wa Worldometer yanaonyesha kuwa ni nchi za India na China pekee zenye idadi ya watu inayozidi jumla ya wafuasi alionao Ronaldo kwenye mitandao yake yote.