@benjekumedia: Kumekuwa na ukosoaji mkubwa dhidi ya uenguaji wa aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam. Katika maoni; Sheikh Mwaipopo amehoji kwa nini viongozi wa BAKWATA walishindwa kulimaliza suala la Sheikh wa Mkoa aliyekuwa ametenguliwa ikiwa ni suala la kawaida la kiutawala na kidini. Ameeleza kuwa Waislamu wanapaswa kuwa na utaratibu wa kutatua changamoto na migogoro yao mapema kabla haijafikia hatua ya kuharibika na kuanikwa hadharani. Kwa mujibu wake, viongozi walipaswa kuyazungumzia na kuyatatua masuala hayo ndani ya taasisi kabla hayajatoka nje. Anadai kwamba kama hatua hizo zingechukuliwa mapema, hata Bella asingefikia hatua ya kuzungumzia suala hilo kwenye mitandao ya kijamii. Ameongeza kuwa kumtengua Sheikh hakujatatua tatizo lenyewe, bali kumeonyesha kwamba viongozi walishindwa kulidhibiti na kulitatua kwa njia sahihi. NB: #Funguka Ungeshilikishwa katika maamuzi ni yapi yangechukua maamuzi yako?!#creatorsearchinsights #tiktok #tiktokindia