@hon_immanuel_mwita: Imefika wakati kama jamii tusimame kidete na kukataa kwa nguvu zote utekaji unaoendelea dhidi ya watoto wetu. Hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha uhalifu huu wa kinyama. Iwe Kenya au Tanzania, utekaji ni uovu unaopaswa kulaaniwa na kila mwenye utu. Cha kusikitisha zaidi ni kuona baadhi ya watu wakiuza dhamiri zao kwa fedha kidogo na kushangilia au kutetea uhalifu huu. Hilo halikubaliki. Maisha na usalama wa watoto wetu si jambo la kufanyia siasa wala biashara. Tuseme kwa sauti moja: Hapana kwa utekaji! Hapana kwa ukimya! Hapana kwa yeyote anayehalalisha uhalifu huu. Na watoto wetu walindwe bila kuyumba. @State House Kenya @Romeo Zungu 1 @Silvanus Osoro, CBS