@abdrash_: "Kukaa kimya si tatizo ikiwa kimya ndio jibu lenyewe, lakini kukaa kimya panapotakiwa kusemwa ndio tatizo." 1. Kimya ambacho ni jibu. Hiki ni cha watu wenye busara. - Unaposhambuliwa bila sababu → kimya kinavunja adui. - Unaposikia gheeba → kimya kinakulinda na dhambi. - Unapokasirika → kimya kinakulinda na maneno utakayojutia. - Jambo halikuhusu → kimya kinahifadhi heshima yako. Mtume ﷺ alisema: "Anayemuamini Allah na Siku ya Mwisho basi aseme kheri au anyamaze" 2. Kimya ambacho ni tatizo. - Unapoona dhulma ikitendeka na unanyamaza. - Unapoona haki ikiporwa na unanyamaza. - Unapoona ndugu yako akipotea na unanyamaza. - Unapokuwa na ukweli unaoweza kuokoa mtu na unanyamaza. Allah anasema: "Na msifiche ushahidi. Na mwenye kuuficha, basi moyo wake ni mwenye dhambi" Q2:283 Nikiwa kimya, nani anaumia? Kama ni wewe tu, kaa kimya. Kama ni wengine, sema. Nikisema, nitaleta suluhisho au fitna? Kama ni fitna, nyamaza. Kama ni nuru, sema. Somo.. Mdomo una nguvu mbili: Unaweza kujenga, na unaweza kubomoa. Na kimya pia kina nguvu mbili: Kinaweza kuponya, na kinaweza kuua. Uwe jasiri wa kusema pale panapotakiwa. Na uwe mwenye hekima wa kunyamaza pale panapotakiwa.
Abdrash
Region: TZ
Thursday 16 July 2026 13:50:43 GMT
Music
Download
Comments
Aisha Ngam :
Tumekuelewa shekhe
2026-07-16 15:33:38
1
Amina omani :
Maa Shaa Allah, wa baarakaallah fiyk shekhe mziwanda mwenyezi MUNGU akuhifadhi na akulinde na Shari za waja wake.
2026-07-16 19:27:46
0
aishanaz :
mashaallah.....mungu akuhifadhi
2026-07-16 17:20:36
0
baisy :
nilitaka kuongea hichhi ki2. ila nikaawa nnasubra sasa mwamba kaongea
2026-07-16 16:03:31
1
roshan msemo :
Mashaallah Jazakallah Ukhaira MwenyeziMungu Akulipe kila lililo la khery 🤲🤲🤲
2026-07-16 14:00:13
1
ngaleni mbwezeni :
eti fulafula dah🤣
2026-07-16 17:38:02
0
ibn umeyr :
😁😁😁 duh fula fula
2026-07-16 18:09:49
0
To see more videos from user @abdrash_, please go to the Tikwm
homepage.