@jacobhoja: Hii ni mfano wa jinsi wataalamu wa jiolojia wanavyotafsiri historia ya mwamba kutoka juu hadi chini. Juu kuna oxidized zone, eneo ambalo limeathiriwa na hali ya hewa na oksijeni. Chini yake kuna saprolite, mwamba ulioanza kuoza lakini bado umehifadhi muundo wake. Kadri drill inavyozama, inafikia parent rock (mwamba mama), ambako ndipo mishipa ya quartz vein huonekana. Ndani ya quartz hiyo kuna visible gold—chembe za dhahabu zinazoonekana kwa macho. Hata hivyo, kumbuka kuwa kuona dhahabu kwenye core si kipimo cha kutosha kuamua thamani ya eneo. Kiwango halisi cha madini kinathibitishwa kupitia sampling, assay na uchambuzi wa maabara. Core drill ndiyo ushahidi muhimu zaidi katika utafiti wa madini. Inaonyesha kina, mwendelezo wa ore body, aina ya mwamba, alteration, na maeneo yenye mineralization, hivyo kusaidia kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuanza uchimbaji. Swali: Je, unajua kwa nini wakati mwingine core yenye visible gold inaweza kuwa na grade ndogo kuliko core ambayo haina dhahabu inayoonekana? 👇
Jacob Hoja
Region: TZ
Monday 20 July 2026 05:03:09 GMT
Music
Download
Comments
Victor Anthony :
umenikumbuka mbali physical Geography 😂
2026-07-20 07:42:41
1
Shaban ⭐ :
💪🛫
2026-07-20 07:29:36
1
To see more videos from user @jacobhoja, please go to the Tikwm
homepage.