@selousfmtz: KAPELA: ANSGAR CUP NI DARAJA LA VIJANA KUFIKIA SOKA LA KULIPWA Mshambuliaji wa zamani wa KMC, Kagera Sugar, Ihefu na Geita Gold, Ramadhani Kapela, amesema mashindano ya Ansgar Cup ni fursa muhimu kwa vijana wenye vipaji kuonekana na kupata nafasi ya kucheza soka la ushindani. Kapela alisema kiwango cha ushindani kilichoonyeshwa na vijana katika mashindano hayo kimemvutia, akibainisha kuwa wapo wachezaji wengi wenye vipaji wanaostahili kupewa nafasi ya kuendelea na safari ya soka la kulipwa. Alisema uwepo wa viongozi na wadau wa soka katika mashindano hayo unatoa nafasi kwa vipaji kuonekana na kuibuliwa. Aidha, amewataka waandaaji kuhakikisha mashindano hayo hayaishii kuwa sehemu ya ushindani pekee, bali yawe na mfumo wa kuwafuatilia na kuwaunganisha wachezaji walioonyesha uwezo na klabu au akademi za soka ili vipaji vyao visipotee. Alisisitiza kuwa maendeleo ya soka yanahitaji uwekezaji, wadhamini na mifumo madhubuti ya kuibua vipaji badala ya kutegemea bahati. Kapela aliyasema hayo wakati akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya Ansgar Cup 2026 yaliyofanyika Peramiho, wilayani Songea, mkoani Ruvuma.

Selousfm Radio
Selousfm Radio
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 20 July 2026 18:57:54 GMT
8490
352
9
8

Music

Download

Comments

sjkdgl3
sjkdgl3 ⚽⚽ :
big up San broo
2026-07-21 11:41:31
0
nasri.mbanga_
Nasri Mbanga_ :
striker la boli
2026-07-21 08:22:33
1
gilbertdesilva4
Gilbert Charles 84 :
Familia yangu
2026-07-21 08:33:02
1
mo_fire48
Mo_fire :
mjomba nakujua kwenye table afai uyo
2026-07-21 06:26:38
1
jemsi.peter
Jemsi peter :
sasa kutaja timu za zamani anakujaje😂😂😂😂
2026-07-21 11:36:05
0
veetruckdriver
❤️🇹🇿Vee Truck driver🚚❤️ :
wakunyumbaaaa
2026-07-21 07:43:45
1
marandu276
LIZABONI ICON 🎒🎒🎒 :
🔥🔥🔥
2026-07-21 07:11:14
0
mo_fire48
Mo_fire :
🔥🔥🔥
2026-07-21 06:27:33
0
userjuniorlaurent
junior@ laurenti :
😁
2026-07-21 15:17:16
0
To see more videos from user @selousfmtz, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About