@seth.jacob88: 🚨 SI KILA KIUA KUVU KINAWEZA KUTIBU UGONJWA! HILI NDILO KOSA LINALOWAGHARIMU WAKULIMA WENGI WA NYANYA. Wakulima wengi hupiga viua kuvu wakiamini kuwa viua kuvu vyote vinafanya kazi sawa. Ukweli ni kwamba, kuna viua kuvu vya kukinga na kuna viua kuvu vya kutibu, na kila kimoja kina kazi yake. Viua kuvu vya kukinga (contact/protectant fungicides) hutumika kabla ugonjwa haujashambulia mmea. Kazi yake ni kuzuia kuvu kuingia na kuenea. Viua kuvu vya kutibu (systemic fungicides) hutumika pale ugonjwa unapokuwa umeanza kushambulia. Huingia ndani ya mmea na kusaidia kudhibiti maambukizi. Ukiona dalili za ugonjwa tayari zimeshaonekana, usitegemee viua kuvu vya kukinga pekee. Tumia kiua kuvu cha kutibu kinachofaa kwa ugonjwa husika, kisha endelea na ratiba sahihi ya kinga ili kulinda mimea iliyobaki. Kumbuka: Kilimo chenye faida si kupiga viua kuvu vingi, bali ni kutumia kiua kuvu sahihi, kwa wakati sahihi, na kwa ugonjwa sahihi. Je, ulikuwa unajua tofauti hii? Andika "NDIYO" kama ulikuwa unaijua, au "LEO NIMEJIFUNZA" kama ndiyo mara yako ya kwanza kuifahamu.
Seth Jacob88
Region: TZ
Tuesday 21 July 2026 17:25:38 GMT
Music
Download
Comments
Godrina George :
pig up 🫡🫡
2026-07-21 18:04:27
0
The Investor :
Asante sana kwa elimu hii. Naomba uzoefu wako juu ya kantangaze, na tuta absoluta n.k.
2026-07-21 20:22:49
0
Ryan :
big up,,unajua sana🔥
2026-07-21 18:05:35
0
Mbozione Mase :
BANKO & CHLOLOPLUS nzuri sana .lakini yaunga ni LIDOMIL
2026-07-21 18:18:54
0
To see more videos from user @seth.jacob88, please go to the Tikwm
homepage.