@gillybonny_tv: Waziri wa Madini, Antony Mavunde, amewataka wachimbaji wadogo na wadau wote wa sekta ya madini kuacha tabia ya kuwaruhusu raia wa kigeni, hususan Wachina, kuingia na kufanya shughuli za uchimbaji kinyume na sheria, kisha kuilaumu Serikali kwa ongezeko lao katika maeneo ya migodi. Mavunde ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wachimbaji wa eneo la Igulula wilayani Nyangwale Mkoani Geita baada ya kuzindua mradi wa umeme katika eneo hilo la migodi. Kauli yake ilifuatia malalamiko kutoka kwa mmoja wa wachimbaji wadogo aliyedai kuwa kwa sasa idadi ya Wachina katika maeneo ya uchimbaji imeongezeka na kuzidi hata wachimbaji wazawa. Akijibu malalamiko hayo, Mavunde alisema Serikali haiwaleti Wachina katika maeneo ya migodi, bali baadhi ya wachimbaji ndiyo wanaowauzia au kuwapa wageni leseni zao za uchimbaji kinyume na utaratibu. "Serikali haileti Wachina. Ni nyinyi wenyewe mnauza leseni kwa Wachina. Sheria za madini zinataka wageni waje kutoa msaada wa kiufundi, si kufanya shughuli nyingine kinyume na sheria," alisema Mavunde. Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia sheria za madini ili kuhakikisha wageni wanafuata masharti yaliyowekwa na kwamba fursa za uchimbaji zinawanufaisha Watanzania kwa mujibu wa sheria.

Gilly Bonny Tv
Gilly Bonny Tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 22 July 2026 08:06:35 GMT
39533
1836
90
124

Music

Download

Comments

beatuslucas327
beatus magigisi :
brother yuko sahihi
2026-07-22 17:07:14
0
temba74051
temba :
kwahii serekali broo hakunaki2 apo ayo wameyaacha hapohapo
2026-07-22 12:42:05
7
paskoo670
kileli :
serekal inabid inunue vifaa vya kuchimbia madin ili wachimbaji wadogo waje na muwakoposhe vifaa hivyo lakin mkisema seria kila kosa mndabadili sheria hapo tatizo halito isha
2026-07-22 10:25:58
3
user3609588172550
Michael :
japhet mwambiga hoja yake isikilizwe
2026-07-22 16:14:18
4
mikodi.ink
mikodiilelo :
kabisaaaaaa
2026-07-24 07:42:01
0
kilimba.lyanga
Kilimba lyanga :
imekaa vizuli hiyo mweheshimiwa
2026-07-22 12:37:21
3
user4278778553851
mtanga zoka kulu :
Tanzania🇹🇿 miaka 30 ijayo Tanzania hakuna wakutushobokea kwakua tutakuwa masikini kuliko na masiki hakuna ane mtaka
2026-07-22 12:10:10
3
cazein26
Cazein26 :
Kwenye madini hatakiwi kua mgeni awe mdogo au muwekezaji mkubwa
2026-07-22 12:13:17
5
kitumbi.daudi
Kitumbi Daudi :
hoja nzr sana ila watekelezaji hawapo
2026-07-22 19:37:26
1
bomani.luhangija
Bomani Luhangija Guguyu :
tatizo watanzania tunashindwa kutambua wachimbaji wadogo ni wapi na manyani ni wapi.?:serikali inaowaita wachimbaji wadogo ni wale wenye maprado na v8 lakin wanaoumia ni hawa watumia moko na koleo
2026-07-22 14:05:27
2
mzawa.dac
mstaafu :
kwan hii nchi inasheria?
2026-07-22 10:43:06
1
nghumbo.malugu.ki
king 👑👑 lyamgoko :
big up sana mh,, umejibu kisomi kbxx
2026-07-22 17:21:04
2
mniko.choma
mniko choma :
kweri wambie jamaa angu
2026-07-22 15:57:28
1
mkamifestus
mkami festus :
kama ninyi ndio wasimamizi wa sheria mmewakamata wangapi kwa kuvunja sheria?
2026-07-23 04:11:25
0
user98853703070
pasco :
wageni wanapitia wapi
2026-07-22 16:39:47
1
amani.amoni
Amani Amoni :
kama shida ni Sheria ibadilishwe
2026-07-22 12:50:03
1
hamid.ndugali3
Hamid Ndugali :
Kwahiyo sheria inaturuhusu tuwafukuze kwa nguvu?
2026-07-22 18:45:38
2
omary.kandi
omary kandi :
umejibu vizuri Sana mkuu wangu
2026-07-22 12:09:12
1
silver_562
Silvanus Meraba♒️ :
Hii ikikua zaidi itabidi tugeuke south africa. Tu amna namna wale walipitia ayaya wakachoka
2026-07-24 12:33:58
0
chachajohn399
William John mron :
kweli
2026-07-23 14:54:17
0
yuukali1
[email protected] :
Safi sana
2026-07-24 03:46:59
0
silver_562
Silvanus Meraba♒️ :
Hatukatai wawekezaj ila wapeme masharti ambayo yanawapa ahueni wazawa
2026-07-24 12:33:17
0
hansernest5
Hans Ernest :
mhhm mambo yamekuwa magum sana
2026-07-23 16:32:00
0
moses.gg94
Moses gg :
Kaka umesema kweli hata hapa nip uganda niivo ivo2 yani 🙏
2026-07-23 19:11:51
0
user3370278680315
FESTO LUVANDA :
tanzanchia
2026-07-22 10:09:23
0
To see more videos from user @gillybonny_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About