@cawabemedia_: Mfanyabiashara mmoja katika Soko la Machinga Complex jijini Dodoma ameibua kilio kuhusu hali ngumu ya biashara, akieleza kuwa ukosefu wa wateja pamoja na mzunguko mdogo wa fedha umeendelea kuathiri shughuli za wafanyabiashara wengi wanaofanyia kazi katika soko hilo. Mfanyabiashara huyo alitoa malalamiko hayo mbele ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, wakati wa ziara yake ya kutembelea Soko la Machinga Complex leo Julai 22, 2026, ambapo alieleza kuwa hali ya biashara imekuwa mbaya kiasi cha wafanyabiashara wengi kutumia muda mrefu madukani bila kupata wateja. “Mheshimiwa, hela ziko wapi? Hela hamna. Unakaa dukani unasinzia kwa sababu hakuna wateja. Mzunguko wa fedha hamna, soko limelemewa,” alisema mfanyabiashara huyo huku akiomba Serikali kutafuta suluhisho la changamoto hiyo. Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, kushuka kwa mzunguko wa fedha kumesababisha mapato ya wafanyabiashara wengi kupungua, jambo ambalo limeathiri uwezo wao wa kuendesha biashara na kutimiza majukumu mbalimbali ya kifamilia na kiuchumi. Akijibu hoja hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema Serikali inatambua changamoto zilizopo, akifafanua kuwa wakati ilipojenga Soko la Machinga Complex haikutarajia ongezeko kubwa la wafanyabiashara waliohamia kufanya biashara katika eneo hilo. Msigwa alisema Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kujenga masoko mengine katika maeneo mbalimbali nchini ili kuongeza nafasi za wafanyabiashara, kupunguza msongamano uliopo katika masoko makubwa na kuweka mazingira bora zaidi ya kufanyia biashara. Aliongeza kuwa upanuzi wa miundombinu ya masoko ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi na kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya kazi katika maeneo yenye ushindani na mvuto wa wateja. Ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali katika Soko la Machinga Complex ilitoa nafasi kwa wafanyabiashara kueleza changamoto zinazowakabili moja kwa moja, huku Serikali ikiahidi kuendelea kusikiliza maoni yao na kuyafanyia kazi kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara nchini.
cawabemedia
Region: TZ
Wednesday 22 July 2026 10:49:32 GMT
Music
Download
Comments
Mkush :
kuna muda mtu anakujibu linakuja tusi kichwani, enewei sawa aisee
2026-07-22 14:03:46
53
Isack Mackphason :
pesa iko wap jibu bwana kashande
2026-07-22 11:32:44
86
Sholah 🥰💫💦 :
Na sio yeye tu pesa hakuna tutabadilisha biashara wangap toeni ela mlikoziweka tunateseka hamjui tu 😭
2026-07-22 17:40:25
19
rITZrOTZ ♊ :
daaah...kqnkumbusha marehem king majuto
2026-07-22 13:52:10
7
Innocent :
mheshimiwa mbona unazunguka jibu swali hela ziko wap?
2026-07-22 17:10:24
13
From your Contacts :
gachagua alipata kusema "uwez kutibu muharo kwa kushona sehem ya haja KUBWA"😎
2026-07-22 15:10:12
6
Ummuh💕 :
NAUMIA SANA MTU ANAULIZWA MASWALA YA NCHI ANAJIB KWA NJIA RAHIS PESA KWEL HAMNA MTAAN IKO HIVI:vitu vimekuwa ghal hivyo pesa inamalizika haraka mishahara midogo haikidhi Hali ya sasa watu wengi wanapoteza ajira kwajili mzunguko Mdogo hivyo kila mtu anaogopa kutumia pesa kwajili yakulinda bajet ya kesho hivyo kuambiwa achie hela ni sawa kwan hakuna haja yakuanzisha maproject tu bila kuangalia wananchi hatuna chakula saiv mteja anakuja na elfu kumi kitu cha 1000 chenji unazunguka adi basi nimawazo yangu sina maana mbaya kwa serekal
2026-07-22 18:32:29
6
LUCY'S STORE KIGOMA :
Atujibu HELA IKO WAPIIIIII mbona ilikuwepooo
2026-07-22 15:45:21
10
Hamis Hamis :
mzee yuko sahihi kabisa yaani mzunguko wa pesa ni mdogo sn shida sio biashara hela hakuna
2026-07-22 14:20:07
10
Annamaria shemahamba🥰 :
Ali ngumu jamani ooh
2026-07-22 12:24:07
14
Vin X5 :
watu wanamwambia Ukweli analeta masihara😁
2026-07-22 14:11:11
4
Herman Ntambala :
unaambiwa hakuna hera unajibu vingine
2026-07-22 15:17:10
3
KILASI INVESTMENT :
kweli kabisaaa😩
2026-07-22 13:17:17
4
BEKA SHOES CLASSIC DODOMA :
swali la msing hela ziko wap
2026-07-22 16:20:00
2
b.ally 🥰.... 🚲 :
Kweli Biashara ni Ngumu hakuna mfano
2026-07-22 17:52:19
1
bisco_supernatural :
kwani hawa watu hawawezi kuongelea mipango ya serikali bila kulitaja exactly jina la rais?
2026-07-22 17:14:23
1
viatu vya shule Dodoma :
😭😭😭😭mwaga pesa wauza viatu ni kilioo😭😭😭
2026-07-22 11:58:37
5
sebastian :
msigwa anafosi maisha yaonekane kawaida
2026-07-22 12:08:01
17
Hassan Nasir jr :
sasa sijui kajibu nini
2026-07-22 16:29:58
1
JULIUS RIMOY :
hakuna kiongozi hapo kwakuwa huyo dada anauza chakula bas watu wote wauze chakula kiongozi hana uelewa wowote kuhusu hali ya mtaani
2026-07-22 17:41:46
1
Mr Pablo 🇹🇿 :
Daaah
2026-07-22 16:10:27
1
Mercedes-Benz Ujerumani :
ubarikiwe mzee
2026-07-22 16:49:00
1
Apollo Ngosha!!!! :
Jibu swali hela ziko wap?????
2026-07-22 15:47:14
7
Mady Issal :
muheshimiwa enyewe anashangaa. elaa🤣🤣🤣
2026-07-22 13:17:35
4
To see more videos from user @cawabemedia_, please go to the Tikwm
homepage.