@chawamata_tv: VIDEO: Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania (CHAWAMATA), Nuhu Mgodoka, amesema changamoto nyingi zinazowakabili madereva wa malori nchini zinachangiwa kwa kiwango kikubwa na madereva wenyewe kutokana na kukosekana kwa umoja, mshikamano na hatua za pamoja katika kutetea maslahi yao. Akizungumza kuhusu mjadala ulioibuka kufuatia taarifa iliyochapishwa na Gazeti la Mwananchi na baadaye kunukuliwa na CHAWAMATA TV, Mgodoka alisema lengo la kurusha taarifa hiyo halikuwa kuhalalisha yaliyomo, bali kuibua mjadala na kuwafanya madereva kutafakari namna taarifa zinazotolewa na baadhi yao zinavyoweza kuathiri juhudi za viongozi wanaowatetea. Alisema badala ya madereva kuishia kubishana kwenye makundi ya WhatsApp na mitandao ya kijamii, wanapaswa kutumia vyombo vya habari kutoa ufafanuzi na ushahidi unaokanusha taarifa ambazo wanaamini si sahihi. Kwa kufanya hivyo, hoja zao zitafika kwa umma na kwa mamlaka zinazohusika badala ya kubaki kwenye mijadala isiyoleta matokeo. Mgodoka alieleza kuwa mara nyingi viongozi wanapowasilisha malalamiko kuhusu mishahara midogo na mazingira magumu ya kazi, hukutana na upinzani pale baadhi ya madereva wanapotoa taarifa zinazopingana na uhalisia wa wengi, jambo linalodhoofisha hoja za kutetea maslahi ya sekta hiyo. Aidha, alisema changamoto za madereva haziwezi kumalizika bila umoja wa kweli, akisisitiza kuwa ubinafsi, kugawanyika na kushindwa kusimama pamoja ni miongoni mwa sababu zinazorudisha nyuma harakati za kudai haki na kuboresha maslahi ya madereva nchini. Katika wito wake, Mwenyekiti huyo wa CHAWAMATA aliwataka madereva kufanya tathmini ya nafasi yao katika mapambano ya kutetea maslahi yao, kushirikiana na taasisi zinazowawakilisha, na kuacha migogoro isiyo na tija ili kujenga sauti moja yenye nguvu itakayosaidia kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya usafirishaji. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #MediaTanzania #OnlineTV #TrendingTZ #TanzaniaTrending #ViralTZ #TeamChawamata #SupportLocal #madeintanzania#madeintanzania #SupportLocal #madeintanzaniat #roadto100followersontwitch #madeintanzaniawith #madeintanzania🇹🇿 #viraltz

CHAWAMATA TV
CHAWAMATA TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 23 July 2026 09:47:44 GMT
18976
530
35
32

Music

Download

Comments

laggabaittamnyama.3
lagga Baitta mnyama204 :
chawamata nao hawajielewi maana safari ya congo anaulizwa dereva wa Loco
2026-07-23 10:07:13
4
swenya.boy
Swenya boy :
hakuna dereva anayeend congo analipwa mil 3
2026-07-23 18:25:05
0
user3370278680315
FESTO LUVANDA :
hakuna mtu anae lipwa milioni 3 ya salufa kutoka daahadi Kongo Yani milioni 2 yenyeewe haifika Mimi nidereva sijawai pata hicho kitu
2026-07-23 11:07:02
0
enockjames693
[email protected] :
nyie chawa ndo mnatuchangany a
2026-07-23 18:47:19
1
benard9964
Beni CHUGA🚬🚬🚬🤣🤣🥽🥽 :
hata siwaelewi chawamata malipo finyu ya madereva lakini mnachokiteteaga naonaniutumbo mtu kiujumla hamna msaada na sisi
2026-07-24 06:41:00
0
abubakarseleman24
mawigi :
chawa aoo awawezi kusimamia DEREVA
2026-07-24 11:32:17
0
side.chotara5
Side Chotara :
midia zinawapanga wasemeivo madeleva
2026-07-24 18:57:49
0
kenethedward5
keneth Edward Halison :
chawamata acheni kuleta tahaluki mnagombanisha watu na family zao nyie ndio chanzo hakuna dreva aliye itwa nyie wauwaji tena wauwaji viongozi uchwara nani kiongozi mmetafuta watu vijiweni ili waongee acheni unafiki
2026-07-23 15:07:32
3
captain_food_
Babylon boy🤠 :
kwani mnaushahidi Gani aliyetoa taarifa hiyo kuwa tunalipwa million 3 ni Dereva wakati ni gaazet ndio limetoa
2026-07-24 04:14:58
0
hoseamagovela1
mago vax :
wale madereva waliohojiwa wafuatiliwe mtafahamishwa vizuri wapo kampuni gani ?
2026-07-23 11:38:54
1
user8304199797366
user8304199797366 :
kwani Hawa chawata wakoupade Gani mana mm naona kamahawana musada nasisi ila wapo kidili lakutuumiza sisi badalaya kututetea Wana tukadamiza ukifikilia mugomo wamwezi wasaba mbona hatokea popote akasimama kuliza hakizamadeleva ziliishiawap Hadi Sasa kanymazatu Sasa mm naona kilamutu afanye awezavyo
2026-07-25 09:42:18
0
omari.ramso
Omari_khan😉 :
gaazeti gani babu hakuna malipo ya milioni 3
2026-07-23 16:51:08
0
noni_maokoto
Hermany Noni :
Maelezo ni mengi, ila ukweli CHAWAMATA ndio wasaliti wa madereva. Iyo taarifa ilivyotoka CHAWAMATA walipaswa waikanushe mapema kwenye page yao kwa masilahi makubwa ya madereva. Ndio mana hata kwenye maelezo ya kwenye hii video bado anawalaumu madereva. 😭😭😭
2026-07-24 18:48:46
0
nyamwezikid
Issa chundu🇹🇿 :
Hao waliolianzisha ndio walimalize sie hatutii neno tumekubali kua tunalipwa milioni 3. kwa kaziyetu ya sulphur na Amoniam ila iposiku mtajua
2026-07-23 10:06:45
0
user3370278680315
FESTO LUVANDA :
kaka Mimi nimefanya kampuni Moja IPO kibahaa nyingine IPO kigambona nampaka saizi nipo nakampuni Moja IPO buza lakini sijawai kulipwa milioni 3 ni 18
2026-07-23 11:10:19
0
laggabaittamnyama.3
lagga Baitta mnyama204 :
kaka maranying mimi nawaonq wanao hojiwa niwale vibaraka tu siyo dereva kwanza kabla kumhoji muulize unaijuaje congo akajib kama kweli dereva
2026-07-23 15:17:31
1
mwinyi.hamadi
Mwinyi hamadi :
babu hamna mnachotutetea nyie jipigieni ela tu ,,,ondoeni taharuki kwenye familia zetu,, uyo unahakika kunadereva aliyehojiwa na ilo gazeti ,,,ondoeni taharuki nyie km viongozi mmepanga tulipwe bei gn kwenye izo sulfa
2026-07-23 17:41:36
1
abushehe08
abushehe :
mimi ndo napewa hiyo mil. 3 lakini napewa kiloho
2026-07-23 18:53:55
0
enockjames693
[email protected] :
awo maderva wa michongo walio ojiwa
2026-07-23 18:48:10
0
user8304199797366
user8304199797366 :
mm naona nijipambanie mwenyewe yakinishinda nachana nakaziyamagali kwani nikizibapacha sitokula
2026-07-25 09:45:41
0
salimukiandiko
salimu :
msitake kututamanishe nyie waandishi wa habar nani anapewa milioni 3 ?
2026-07-24 06:51:10
0
baita.ommy
Ommy truck driver :
hapana naongea hapa nipo sakania ni uwongo huo 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
2026-07-23 16:15:36
0
nenguni16
Neng'uni :
Wekemia walivyo jikinga wamevaa mitungi ya Hewa .na dereva ana lala kwenye kibini miezi miwili.Tutawaacha watoto wakiwa mayatima kwa faida ya matajiri .Dereva yafaa hiyo kazi aifanye kwa muda mfupi na aachane nayo na kwenda kijijini kulima vinyungu .Kongo dereva alipwe Milioni 7.😳
2026-07-23 12:06:08
1
tareeq_aziz
tareeq aziz :
😅😅😅
2026-07-23 17:29:35
0
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About