@pancreascare1: Kisukari ni changamoto ya kimetaboliki ambayo inatokea pale ambapo mwili unashindwa kutumia sukari (glucose) vizuri kutokana na upungufu wa insulini au mwili kutoitikia insulini ipasavyo. ➡️ Kongosho (pancreas) ndicho chombo kinachozalisha insulini — homoni inayosaidia sukari kuingia kwenye seli za mwili kwa ajili ya nishati ➡️ Kisukari kinatokea pale kongosho linaposhindwa kuzalisha insulini ya kutosha, au mwili unaposhindwa kutumia insulini vizuri ➡️ Kadiri kongosho linavyoendelea kulemewa, uwezo wake wa kuzalisha insulini hupungua taratibu ➡️ Kujua chanzo hiki ndio hatua ya kwanza ya kudhibiti na kuzuia kisukari kabla halijaendelea Kuna aina kadhaa za kisukari, lakini leo nataka nizungumzie zaidi kuhusu Type 1 na Type 2. ➡️ Type 1 — kongosho haliwezi kabisa kuzalisha insulini; mfumo wa kinga ya mwili huathiri seli zinazozalisha insulini. Aina hii huanza mara nyingi utotoni au ujanani ➡️ Type 2 — kongosho bado linazalisha insulini, lakini mwili haujibu ipasavyo (insulin resistance), au uzalishaji hupungua taratibu kwa muda. Aina hii huhusiana zaidi na mtindo wa maisha, mlo, na uzito ➡️ Type 2 ndiyo aina inayoongoza duniani na inaweza kuzuiwa au kudhibitiwa kupitia mabadiliko ya mlo na mtindo wa maisha Kwa maelekezo zaidi kuhusu kisukari, jiunge na PROGRAM yetu ya WhatsApp. 📲 #kenyantiktok🇰🇪 #congolaise🇨🇩 #usa🇺🇸 #deabetes #pancreas

PANCREAS CARE 🙌
PANCREAS CARE 🙌
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 23 July 2026 14:40:01 GMT
1251
9
0
1

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @pancreascare1, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About