@veriafya: Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetangaza kutoa huduma za uchunguzi, tiba, chanjo, na elimu ya afya ya ugonjwa wa homa ya ini bila malipo kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Homa ya Ini Duniani. Maadhimisho hayo yanayofanyika Julai 28 kila mwaka, yanalenga kuongeza uelewa na kupambana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo nchini. Akizungumza kuhusu mkakati huo, Daktari Swalehe Pazi Bingwa wa Mfumo wa Chakula na Ini kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo Kliniki ya Muhimbili Sokoine Drive Medical Centre (MNHSDMC), iliyopo mkabala na barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam ili kupata huduma hizo muhimu na kujua afya zao mapema