@kusagatv: MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 25 AKUTWA AMEFARIKI DUNIA NDANI YA NYUMBA YAKE ARUMERU Arumeru, Arusha – Julai 29, 2026 – Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Elizabeth Frank Kimsangi, mwenye umri wa miaka 25, amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake iliyopo Kitongoji cha Oltulelei, Kata ya Ilboru, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha, katika mazingira yanayozua maswali. Mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umefunikwa kwa zulia, huku damu nyingi ikiwa imetapakaa ndani ya chumba. Kwa mujibu wa taarifa za awali, mtu anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo alitoroka mara baada ya tukio hilo kutokea. Mashuhuda wanasema mwendesha bodaboda ambaye alikuwa akimpeleka marehemu kazini mara kwa mara ndiye alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika nyumbani kwake asubuhi. Alieleza kuwa alipowasili alikuta mlango wa nyumba ukiwa wazi. Alipoingia ndani aliona damu kuanzia mlangoni na baadaye akaukuta mwili wa Elizabeth ukiwa umefunikwa kwa zulia. Inaelezwa kuwa marehemu alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja ya utalii jijini Arusha. Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi na taratibu nyingine za kisheria. Uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwabaini waliohusika.
MWANDISHI WA WANANCHI
Region: TZ
Wednesday 29 July 2026 10:36:46 GMT
Music
Download
Comments
Rebby :
Yan leo arusha nimeona hii taarifa ya pil mara mwanmke kamchoma mumew koromeo 😢
2026-07-29 11:16:25
127
naju :
Arusha is too much sasa
2026-07-29 11:00:37
50
ester apple :
Eliza jamn 😭😭
2026-07-29 14:32:27
0
jordanahmolly :
Eliza jaman why so early 😭😭😭
2026-07-29 14:39:52
0
Eric Moshi :
Arusha wakuu this is too much daaah
2026-07-29 11:51:40
0
Mwaisa Tanzania 🥑🥑 :
the city of events 😭
2026-07-29 12:37:24
0
🦁👸 :
Jehovah🙂↕️
2026-07-29 11:18:39
1
user3463594861303 :
Ila Arusha Wana confidence ya ajabu 🥹😭😭
2026-07-29 12:01:33
0
Glory Christian :
kwanini arusha kila siku mara huyu kamuua yule mara ivi why
2026-07-29 11:05:46
24
omybebe1♋️ :
Asubuhi na usiku mnapokuwa mna sali kwnye maombi yenu msisahau kuombea Arusha aise😓😓😓😓😓😓😓
2026-07-29 11:12:56
4
🦋Natthy Montannah🙈💦 :
KAMA INAWEZEKANA SERIKALII IINGILIE KATI JIJI LA ARUSHA LIINGIZWE KWENYE MAOMBI NA MASHEKHE NA MAPADRII HII IMEZIDII SASA🥹🥹🥹🥹🥹
2026-07-29 13:13:28
2
Mamusca :
Arusha Mungu asimame nao
2026-07-29 11:17:39
5
malechela :
jaman Arusha Kuna nn tenah mbn watu wanauliwa
2026-07-29 14:58:24
0
perfect :
mmmh ARUSHA mbona matukioh mengi jamani Kuna mama Jana tena kamwangiwa mafuta yamoto 🤔🤔🤔🤔
2026-07-29 11:55:08
4
mery.kikwale :
duuh Arusha kwa matukioo Yesu aikumbuke😭
2026-07-29 14:06:00
1
chita girl :
ila Arusha🙌
2026-07-29 11:37:17
2
shebyboy😎🤫👊 :
Unajua kuna mda mpaka naaza kuogopa Hii Arusha yangu dah 😓😓🤔🤔
2026-07-29 13:17:09
1
Maggie :
sijui nihame Arusha mbona matukio Ni mengi jamani We MUNGU tusaidie.
2026-07-29 11:10:28
12
Amos Nyamaka :
arushaaaaaa
2026-07-29 11:32:18
1
𝓲𝔃𝓮𝓻🔆 :
Ni mbaya enyewe
2026-07-29 11:47:50
1
Queen bee :
hivi Arusha mnatuleteaga na taharifa za miaka ilopita au ni nini mbona matukio kila kukicha na yakutisha ni Arusha jamani
2026-07-29 12:18:26
1
Jacqueline007 :
2026-07-29 11:28:31
1
Mary Mselle :
yaani mungu asimame sana Arusha, maana kila tukio Arusha.
2026-07-29 11:16:17
5
Mamosi12 :
Duu,Arusha kuna nini lakini
2026-07-29 11:57:07
1
To see more videos from user @kusagatv, please go to the Tikwm
homepage.