@playstation_storetz: 🎮 SONY YATAJWA KUTENGENEZA CONTROLLER ZA KUGUSWA KAMILI Kampuni ya Sony inatajwa kuwa inafanyia kazi teknolojia mpya ya controller za PlayStation ambazo zinaweza kudhibitiwa kwa kutouch moja kwa moja badala ya kutumiabutton za kawaida. Kwa mujibu wa taarifa zinazozunguka mtandaoni, controller hizi zinaweza kutumia touchscreen au eneo kubwa la kutouch, hivyo kuruhusu wachezaji kufanya vitendo mbalimbali kwa kugusa, kupangusa (swipe) au kubonyeza sehemu tofauti za controller. Lengo ni kuongeza ubunifu katika uchezaji na kuwapa watumiaji uzoefu mpya wa michezo. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa hadi sasa Sony haijatangaza rasmi kuwa controller hizi zitaingia sokoni. Kinachoonekana ni hati za ubunifu (patents) na dhana (concepts) zinazoonyesha mwelekeo ambao kampuni inaweza kuufuata siku zijazo. Iwapo teknolojia hii itazinduliwa, inaweza kubadilisha jinsi wachezaji wanavyocheza michezo ya PlayStation kwa kuondoa baadhi ya button vya kawaida na kuongeza njia mpya za kucheza games Je, wewe ungependa kutumia controller ya touchscreen, au unaona controller za sasa zenye button bado ndizo bora? 👇🎮 . . . . . #tanzania #fyp #tanzaniatiktok #simbasc #yangasc

Playstationsstore_tz
Playstationsstore_tz
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 30 July 2026 02:44:42 GMT
6592
204
9
36

Music

Download

Comments

khizer.daud0
ķĥáĺèed🦅 :
hawapo serious 😂
2026-07-30 10:19:14
0
47r4sh
47R4§H :
hapana lazima waweke physical buttons
2026-07-30 10:45:12
0
peterkimi100
Peter kimi :
Sasa ni nn hii 😂 kuna wale wakubonyeza kwa nguvu apa lazima screen ivuje wino 🤣🙌🏽
2026-07-30 09:06:34
3
fleimz
Ceejay 😎 :
Screen zitatufia waafrika😂
2026-07-30 10:29:56
0
ellyluck
ellyluck :
hiyo bei sasa tecno ya mtu😂😂
2026-07-30 10:25:16
0
ferooz19862003
FEROOZ 👑🇹🇿🇦🇪🇬🇧💕 :
wamezingua
2026-07-30 08:40:32
0
young.hinya
Young Hinya :
mbaya hiyo wamehalibu
2026-07-30 07:23:27
0
nizaryamory001
نيزاري أموري :
saiz mambo X haifanyi kaziii
2026-07-30 06:53:22
0
To see more videos from user @playstation_storetz, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About