@cawabemedia_: Msemaji wa Timu za Taifa, Haji Manara, amemtaka aliyekuwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta, kutafakari upya uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa na kurejea kuichezea timu hiyo kwa ajili ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Julai 30, 2026, Manara amesema alishtushwa na taarifa ya Samatta kutangaza kustaafu kuitumikia Taifa Stars, akieleza kuwa mshambuliaji huyo bado ana uwezo na mchango mkubwa kwa timu ya taifa. Amesema ushiriki wa Samatta katika AFCON 2027 ungekuwa hitimisho zuri la safari yake ya kuitumikia Tanzania, hasa wakati nchi itakapokuwa mwenyeji mwenza wa mashindano hayo pamoja na Kenya na Uganda. Manara ameongeza kuwa endapo Samatta atakubali kurejea, kutafanyika maandalizi ya mechi maalumu ya kumuaga kwa heshima, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa kwa Taifa Stars na soka la Tanzania. Aidha, amependekeza jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Samatta istaafishwe kwa muda, hata kama ni kwa mwaka mmoja, kama ishara ya kuthamini mchango na historia aliyoandika akiwa na timu ya taifa.

cawabemedia
cawabemedia
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 30 July 2026 14:24:21 GMT
27463
1034
37
5

Music

Download

Comments

user7441848141218
Chris :
Wachezaji wapo wengi sana mtu ametangaza kustaafu mwacheni bado mnambembeleza wa nn nchi inawachezaji wengi yy wakati wake umepita acheni kuleta siasa kwenye mpira kwanza sasa hivi mchango wake umekuwa mdogo wapo vijana wenye nguvu na nia ya mafanikio acheni kusema watanzania wanamuhitaji kinanani hao acheni siasa bwana.
2026-07-31 01:45:27
5
user6238255838260
justice .... :
samata ni mchezaji bora afrika mashariki akuna wakufananishwa nae
2026-08-02 10:55:19
0
hamphrey17
Humphrey17 :
kuna kitu tunashndwa kumuelewa manara anacho manisha ni sawa na kijiji akikosi wazee ko samata ni sawa na mzee kwenye kijiji ata asipo cheza atakua na maneno ya busara kwa wachezaji wengne watakapo kua vyumbani au pale benchi...🙏
2026-08-01 04:51:47
1
jayvanny_6
jayvanny_6 :
once not twice
2026-07-31 10:26:12
1
user3622718897309
gift kisyuka :
leo nimeemuelewa sana manara kwa factor hio
2026-08-01 21:34:03
0
user1293629088281
salumabdallah :
usikubali Samanta cc watanzania hatuna jema ulishatukanwa sana,kuwa na msimamo
2026-08-01 09:14:42
0
agunashi
lameck :
watanzania na nani
2026-08-01 07:12:24
0
simon.lupungu
Simon Lupungu :
kwa mtu yoyote anaelewa football ataungana namanara na kila.mtu.anaetaka.samatta.akudi.kwenye afcon itakayocheza afrika.mashariki hapa
2026-08-01 05:05:50
0
lastminites90
Lastminites :
😂😂😂 Jaman hiki nn sasa
2026-07-31 23:55:28
0
user92558140299814
adi :
achananeni nae bhna
2026-07-31 16:17:19
1
ukwelimchungu2
MR.X :
Hamjawahi kumtetea pale watu wasiojuwa mpira wakimtupia maneno ya kumvunja moyo...Heshima ya Samatta mnawapa Watu wasio sahihi na kumfifisha na kumlinganisha na wachezaji wasio na hadhi..
2026-07-30 20:34:12
4
che.guevara9597
che guevara :
mnamzarau kisha mnamuomba
2026-07-31 21:32:32
1
matabala1
Matabala 🇹🇿 :
Hii ndyo Tanzania 🇹🇿nchi yangu 🙌🙌 samata huyu huyu haibebi team ya Taifa....na maneno kibao....leo kaomba akae pembeni ili vijana waoneshe vipaji vyao 🤣🤣
2026-07-31 19:26:47
1
hashimissa2
Hashimmoh’d :
Ahh aende tu 😁😁
2026-07-30 16:15:27
0
somby.khalidy
Somby Khalidy :
hii tabia ya kuomba mchezaji nikizamanisanaa mtu aachie timu wengne wapambane
2026-07-31 10:59:08
0
gaudence4050
GAUDENCE4050 :
m namuomba asichezee abakii tutoe wachezaji wengine hapo vp w2 wa mpira?
2026-08-01 11:02:05
0
atsalsule
Atsalsule :
mutamuomba mpk lini , acheni siasa emu , sio kwa ubaya
2026-08-02 01:46:25
0
mnyepe.matelephone
MNYEPE STORE :
kwan hakuna wengn mpka captain uyo kashachoka tumpe heshima yake bhas
2026-07-31 07:36:51
1
omaryvikashi
vikash jr :
Hakuna namna kila zama na wakati wake ni wakati sahihi sasa mbwana Ally sammata kuachia vijana bado tunasafari ndefu sana ya kujenga team ya taifa ila kwenye kujenga team ni subra ni hekima sammata kupisha vijana na vijana tunao wa kujenga team tuwape muda vijana
2026-08-20 07:31:48
0
adallah.rashid.md
Adallah Rashid Mdiliko :
kweli awesome ni icon kubwa
2026-07-31 04:01:07
0
vascodezanzibar
de zanzibar :
Tengenzeni kina samatta wengine sio kulazimisha mtu ambaye akiwepo ajitumi
2026-07-31 07:24:49
0
omaryramadhani297
omaryramadhani297 :
kiukweli mmi sija muomba kabisa japo yuko vizuri Samatta ila maamuzi yake ya heshimike
2026-07-31 12:12:49
0
user6155187005049
MHUNZI IGOSO :
ndio mnaharibugi timu Ivo mnalazimisha vitu ambavyo haviivitajiki
2026-07-31 08:48:43
0
nomasanadj
dj daru tz :
uyo samata ndonani wachezaji wote ao
2026-07-31 17:27:32
0
gotama.mtandi
Gotama Mtandi :
wew kocha nyie ndio mnahalib mpira wa tanzania
2026-07-31 03:12:39
1
To see more videos from user @cawabemedia_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About