@paza_sauti_media: Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, amemsimamisha kazi Mwenyekiti wa Kitongoji cha Maguruwe, Kata ya Msimbu, Saidi Fundikila, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, ikiwemo kumpiga Mwananchi, Athuman Kizoka, kumfunga pingu za Polisi katika Ofisi ya Kitongoji kinyume cha sheria, kumiliki pingu hizo bila uhalali, pamoja na kupora nyumba ya Mama wa Athuman. Inaelezwa kuwa, Mwenyekiti huyo alijichukulia hatua hizo baada kufuatia madai ya Shilingi Milioni 3.3 kutoka kwa Athuman Kizoka, akidai fedha hizo zilihusiana na mzigo aliomtuma Kijana huyo kuufuata kupitia Mwanaye ambao ulipotea. Wananchi walidai kuwa katika kufuatilia deni hilo, Mwenyekiti huyo alimshambulia na kumpiga Athuman, akamfunga pingu ndani ya Ofisi ya kitongoji, kisha akachukua nyumba ya Mama yake kama dhamana licha ya kutokuwa mali ya mdaiwa. Akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi uliofanyika Julai 29, 2026 katika Kitongoji cha Maguruwe, Magoti alisisitiza kuwa Serikali haitaendelea kuvumilia matumizi mabaya ya Ofisi na madaraka yanayowanyanyasa Wananchi na kuzalisha chuki dhidi ya Serikali badala ya kutatua matatizo yao, akieleza kuwa viongozi wote watakaobainika kufanya vitendo vya aina hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Paza Sauti
Region: TZ
Thursday 30 July 2026 17:15:56 GMT
Music
Download
Comments
mkenya og :
simpendi uyu baba
2026-07-31 07:16:06
9
Jamali Kimaro :
mwenye kit wa mtaa atenguliwi kaka huyo kachaguliwa na wananchi acha wengeee
2026-07-30 18:39:07
35
nassa mawe :
mwenye kiti anachaguliwa na wananchi mkuu wawilaya anateuliwa
2026-07-30 18:11:46
9
jeremiah Daniel :
umetisha kaka Magoti congratulation
2026-07-30 20:23:39
0
pelikani_med F.N :
mkuu wa wilaya hana mamlaka yakumsimamisha mwenyekiti
2026-07-31 01:24:07
8
France.. :
mimi huyuu hata kma akinisimamisha kesho laazima niendee kazini atanifanyaje sasa huyu
2026-07-30 19:13:18
8
mathius :
kwa utashi wangu najua mwenyekiti huchaguliwa na wananchi na hitenguliwa na wananchi
2026-07-31 05:50:42
2
Shafii mashono :
mkuu wa wilaya anayoo mamlaka ya kumsimisha mwenyekitu Kwan anafanya kazi chini yake ingawa ameteuliwa na Wananchi
2026-07-31 08:31:59
1
simple but heavy :
mwenyekiti kukaa na pingu ni kawaida maana ndio mwenye ulinzi na usalama ndani ya eneo lake kama migambo wanakuwa na pingu sembuse mwenyekiti
2026-07-30 18:53:01
9
user579000341262 :
kikatiba hana mamlaka ya kumtengua mwenyekiti kwan amechaguliwa na wananchi Kwan yy ameteuliwa na Rais
2026-07-31 08:27:48
2
h kiwa mo 12 :
sio Kwa ubaya kwani mwenyekiti sikuiz wanateuliwa au, anatenguliwa vip wakat amechaguliwa na wananchi
2026-07-30 20:42:29
3
freshboyz🇹🇿 :
mkuu wa wilaya ana mamlaka ya moja Kwa moja kumsimamisha kazi mwenyekiti wa kitongoji Kwa maamuzi yake pekee Kwa sababu ana chaguliwa na wananchi
2026-07-30 18:24:13
5
𝐒𝐚𝐚𝐝𝐚👑 :
kiukweli nampenda huyu mkuu wa wilaya nataka anioe jamani
2026-07-31 06:09:45
1
moh'd :
Hapo mwenyekiti anapisha uchunguzi Na sio kufukuzwa
2026-07-31 07:00:33
0
dvj Bimbim :
angalia wananchi/ angalia na kiongozi🥺
2026-07-31 08:41:58
1
user58853013705574 :
Nakupenda sana Mkuu unasimamia haki.
2026-07-31 11:24:41
1
Gloris Ndawa :
😳ila siku hizi kweli umsimamisheje aliyechaguliwa na watu uwiiiii
2026-07-30 19:07:27
1
Tauhidi Rukokerwa :
kwer bana
2026-07-30 21:43:02
0
GASPER KISINZA :
Viongozi wanapaswa KUPATA MAFUNZO YABUONGOZI NA UTAWALA
2026-07-31 16:21:49
1
Home boys :
Kwwnye ichi hii sioni umuhimu wa mkuu wa wilya wala mkuu wa mkoa
2026-07-31 04:46:01
1
bakar :
KISHERIA MH, MKUU WA WILAYA NDIO MWENYE MAMLAKA YA KISHERIA YAKUMSIMAMISHA M/KITI, ILA KWA UTARATIBU UFUATAO ,KISHERIA, UTAITISHWA MKUTANO MKUU WA WAKAZI WA MTAA HUO, NIKAMA ALIVYOSEMA HIYO TUHUMA, KISHA ANARUDISHA KWA WAKAZI.HUSIKA, KWA.KUPIGA KURA, KWA KUPATA IDADI WANAOSEMA , ASIMAMISHWE KAZI AU AENDELEE, KWA.VIDOLE HADHARANI KISHA MKUU WA.WILAYA ATATANGAZA.KUNDI LILIO SHINDA ,ILA KWAHAPO MAAMUZI HAYO KAJANAYO YEYE MH, M/KITI AKIENDA MAHAKAMANI ANARUDI FASTA NA MAJUKUMU YAKE
2026-07-30 19:15:20
1
Mgosi :
kwani mwenyekiti si anachaguliwa na wananchi au mm ndio sijui😳😳😳
2026-07-30 22:02:19
0
To see more videos from user @paza_sauti_media, please go to the Tikwm
homepage.