@talkboutitwithconradley: Unpopular opinion! Hii content imenipa uzito sana kuitoa kwasababu ya mtazamo wa jamii, na tukubaliane sio content ya kila mtu, kuna watu itawaudhi na kuwafanya waone sio kitu cha kuzungumziwa in public na mtu mwenye ushawishi kwa watu, ila ni vyema ifike sehemu tuambiane ukweli unaouma na ambao hatutawahi kuuzowea kutokana na kofia iliyovikwa "NDOA". Ndoa imevikwa kofia ya "utakatifu" ni kitu chema, especially kwa wakristu (sipingani na hilo) ndio maana imekua ni kitu cha laana, kushindwa na kuonekana hujakamilika pale imetokea ndoa yako imeshindikana. Vitu vyote vyenye hiyo kofia vimekua vigumu sana hata kwa watumishi wa Mungu kuvivunja kwasababu inaonekana unaingilia kilichojengwa na Mungu, nyumba za ibada haziwezi kukushauri kwamba hii ndoa sasa imefika mwisho think otherwise, imekua inaonekana kama wanaingilia kusudi la Mungu. Swali dogo la kujiuliza ni..hawa watu takribani 130 wanao uw@w@ kila mwaka wakiwa kwenye ndoa kusudi lao mbele za Mungu lilikua ni nini? Kama Mungu aliwapa akili ya utambuzi, kuelewa na uwezo wa kufanya maamuzi, kwanini walishindwa kuona ndoa zao tayari zilishashindikana, wakaamua kusubiri vi£o vyao visababishwe na wenza wao kwenye ndoa kwa kuogopa kuwa judged na jamii. Jamii imeendelea kujitoa kwenye huu "ubaya" wa kuvunja ama kushauri watu waachane na ndoa zao mbaya. Familia zimeendelea kuwasukuma wapendwa wao kwenye ndoa mbovu kwa kuona aibu kuwa "wataonekanaje" pindi watoto wao watakapoonekana kashindwa kuishi kwenye ndoa zao. Ni hadi pale kijana wao anapo-uw@w@ ndio utaona machozi na majuto ya kila aina na unafiki wa kwamba tulijua na tulimshauri aachane na lile shetani..mume/mke. Ifike sehemu tuzungumze na watu wetu wa karibu ukweli, tuwaambie bila aibu kuwa ndoa zao zilipofika ni vyema kujiongeza bila kusubiri kuhudhuria misiba yao, waangalie nje ya box bila kujali familia na jamii watasemaje. Sidhani kama kusudi la Mungu ni kuona anatumia chombo chake mwenyewe "ndoa" kuangamiza watu wake, ni watu wake wameendelea kuangamia kwa kukosa maarifa. "Watu watanionaje" umekua ni mstari ambao unatumiwa na wanandoa wengi sana ambao leo tumebaki na kumbukumbu zao makaburini. NIMEAMUA KUWAFUNDISHA KILA KITU! #lifelessons #life #tiktok #tiktoktanzania🇹🇿 #tiktokkenya🇰🇪

talkboutitwithconradley
talkboutitwithconradley
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 01 August 2026 06:10:01 GMT
16623
1415
47
66

Music

Download

Comments

giana20
Gian shop store :
hii yangu sijui kama ni pingu au gereza soon nabeba vifaranga wangu
2026-08-01 06:45:52
10
naahmohd09
N@@h🎆 :
me ndio stk kupitia mabalaaa ni bora niwe huru🤣🤣🤣🤣
2026-08-01 06:28:05
2
chi.mama5
chi mama :
😭😭😭😭 sitamni Tena sizani kama nitarudia ten
2026-08-01 22:08:56
0
user7707217082161
elen Mohamed :
kaka hapo umenena , maumivu yaliyopo ni kilio kila siku nakosa ata maana ya ndoa naona kama ni uwanja wa vita, mtu anakwambia vumilia ili ulee watoto ,amani , furaha haipp tena ndoa hiziiiiiii, mungu asimame maana nishachoka vibayaaa
2026-08-01 21:02:34
2
flr2010f
flr :
mimi baada ya kugundua tunaishi mara moja tuu na kama siku ikipita imepita na haijirudiii kamwe kwnye maisha yako...basii i love myself naish kivyangu na kama sina furaha na aman basi nakupisha upite na sikuwazii kamwe..Maisha ni mafupi mno kukubali kupoteza muda wako kwa ajili ya kiteseka😅
2026-08-02 02:02:59
1
stoicphina
STOIC MEDITATION :
Waah ...noma sana
2026-08-02 06:27:10
0
eulalia.gerald
Eulalia Gerald :
yangu Haina jina yooooo! 🤲🤲
2026-08-01 13:56:56
0
sikituwakulu
Sikitu Wakulu :
eemungu ndowa nimetumikia aswa ila nimeshindwa
2026-08-01 19:01:36
1
user73131001998720
mom mina 💦💦 :
nakumbuka nilikataa kuolewa siku moja kabla ya harus nashukuru mmung maan huwa nakaa najiulza lait ningeingia kwenye ile ndoa sijui future yangu ingekuwa wap leo usikute hat hii video nisingeona waty wanateseka kwel watu wanapitia magumu mno san nimekuwa muoga now kwa kila kitu mahusiano ndoa nimekuwa muoga sana
2026-08-01 13:12:02
1
neemanasua
Neyney flowers :
aisee umeongea kweli sana
2026-08-02 02:47:34
0
noelapascal707
Noela Pascal :
kaka ukweli kabisaaa
2026-08-01 09:54:24
0
officialcareen06
mrs. no body🧸 :
Mungu nijaalie me na wangu tukifunga ndoa iwe ya aman japo kuna mikwaruzo ila isiwe kerooooo😅😂😂😂😂😂😂😂
2026-08-01 15:39:04
1
alicedevase
Alice_azzle🦋🙊🌸 :
💯
2026-08-01 06:15:50
0
1777mu
shoni :
apo ndio utajua ndoa huwa aina umuhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu ni kitu cha ziada tuu
2026-08-01 17:11:37
0
mamy.faith0
Mamyfaith :
Kaka umeongea point kubwa sana,,Watu wanateseka kwenye ndoa na wanaogopa kutoka,kisa familia,kisa dini itanionaje,,kisa jina ,,mi nilishatoaka huko sijaja duniani kuteseka kwishaaa.
2026-08-02 04:59:40
0
kheighlybright69
user1264962788687 :
Uko sahihi kaka,ikiwa mambo yamerekebishwa mara nyingi kwenye ndoa na hakuna mabadiliko ni bora kuachana kuliko kufa.
2026-08-01 07:38:03
0
miss.rachelchrist
miss Rachelchristian :
pingu za maisha daah 🙌
2026-08-02 06:54:38
0
monnah237
Monnah❤️ :
Yanii apa umeniongeleaa mimi kabisa yesuu 😂naishi kama mchawiii
2026-08-01 11:12:01
1
kichinchiri
Latifah :
Kweli kakaa
2026-08-01 13:33:25
0
love..family6
LOVE..FAMILY❤️❤️ :
nisiseme sana🤐
2026-08-01 11:12:04
0
butterflysally0
butterflysally0 :
Ngoja niwaze kwanza
2026-08-01 06:22:08
0
To see more videos from user @talkboutitwithconradley, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About