@zbc_zanzibar: Wakati changamoto ya ajira ikiendelea kuwakabili vijana wengi nchini, hali ni tofauti kwa vijana wanaofanya kazi katika Shamba la Viungo Mwera Pongwe, Zanzibar, ambapo wamepata fursa za ajira zinazowawezesha kujipatia kipato na kujitegemea kiuchumi. Wakizungumza na ZBC, vijana hao wamesema mbali na kushiriki katika shughuli za utengenezaji wa kofia za asili na bidhaa nyingine zinazovutia watalii, kazi wanazozifanya zimekuwa chanzo cha kipato kinachowasaidia kukidhi mahitaji yao pamoja na familia zao. Aidha, wamesema sekta ya utalii imekuwa daraja muhimu la kufungua fursa za kiuchumi kwao. Vijana hao pia wametoa wito kwa wenzao kutumia fursa zilizopo katika sekta za kilimo na utalii kwa kujiajiri na kujitafutia kipato, badala ya kusubiri ajira za Serikali pekee. Wamesisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza umaskini, kuboresha maisha na kuwaepusha vijana na vitendo vinavyoweza kuhatarisha mustakabali wao. 📹 Mwandishi: Asha Hassan #ZBCUpdates
ZBC Zanzibar
Region: TZ
Saturday 01 August 2026 11:10:50 GMT
Music
Download
Comments
L'homme Seul 😔 :
Sio Mwera Pongwe Ndugu Mtangazaji 😂😂
Ni Dole Spice farm or Kizimbani Spice farm
2026-08-02 06:23:18
2
^KHAMIS->♤♤♤ :
vijana tunajiajiri lakini kila siku kodi zinapanda mapaka skuizi kazi ya utalii ishakuwa ngumu..
2026-08-01 21:32:02
2
Gabriel de zanzibar🇦🇩🇦🇩 :
Kodi mpaka Zina kaba unakosa atapesa ya kufanya mambo ya muhimu so kwaiyo serikali iangalie hili kwasababu ikiona hivi ndo inaleta kodi zaidi wakat vijana tunajiajili wenyewe
2026-08-02 04:26:22
1
bigi mohd :
mulizeni. kiwanja chake kipo wapi
2026-08-05 14:05:11
0
Abdiy02 :
sio mwera apo
2026-08-02 17:30:41
0
Island soul & safari :
umoumo tunamo jiajiri tunaekewa pingamizi
2026-08-02 06:17:35
1
mwazini Brand :
good 👍
2026-08-01 20:47:13
0
Mr ZANZIBAR :
mwera tena jmn mbn sielwi
2026-08-02 18:59:59
0
Ibrahim Z'bar :
Hiyo sio Mwera Pongwe
2026-08-02 16:13:58
0
hamsi balığı zanzibardan :
mm nasema nitano tena ndo ninachofahamu 😆😆😆😆😆😆
2026-08-02 06:18:54
0
Abuu :
heeee bora nikae kmy tu
2026-08-01 18:43:08
0
mansor juma 🥰 :
shaban
2026-08-02 06:26:22
0
iliamoh Zanzibar safar :
ndugu mtangazaji hii ni dole sio mwera pongwe
2026-08-03 05:37:06
0
HGsultan :
Huyu mmoja mbn anachekaa 😂😂
2026-08-02 04:47:12
0
njuma :
pastoree mkanyagenii hyoo
2026-08-03 06:09:38
0
To see more videos from user @zbc_zanzibar, please go to the Tikwm
homepage.