@iconglobal8: "Walichimba kwa miaka zaidi ya 20 wakitaka kujua kilichopo chini ya dunia… lakini walichokutana nacho kiliwalazimisha kusimama mara moja." Mwaka 1970, wanasayansi na mainjinia wa Urusi walianza kuchimba shimo refu zaidi kuwahi kufanywa na binadamu, lililokuja kujulikana kama Kola Superdeep Borehole. Lengo lao lilikuwa kufahamu siri zilizofichika ndani ya dunia. Baada ya miaka mingi ya kazi, walifanikiwa kufika zaidi ya kilomita 12 chini ya ardhi. Lakini walipofika huko walikumbana na joto kali lililofikia karibu nyuzi joto 180°C, hali iliyoharibu vifaa vyao na kuwalazimisha kusimamisha mradi mwaka 1992. Katika kina hicho waligundua maji yaliyofichika ndani ya miamba na mabaki ya viumbe vya kale. Baadaye, simulizi zikaanza kusambaa kwamba lilikuwa njia ya kuelekea kuzimu" kutokana na madai ya sauti za ajabu kutoka ndani yake. Lakini ukweli ni kwamba Kola Superdeep Borehole lilibaki kuwa ushahidi wa jinsi binadamu alivyojaribu kufungua siri za ndani kabisa za sayari yetu. karibu ICON Global Podcast nyumba ya simulizi zilizoacha alama #tiktokuganda🇺🇬🇺🇬🇺🇬 #tanzaniantiktok🇹🇿 #tiktokkenya🇰🇪 #viralvideo #congolaise🇨🇩