@power_media08: MAXI NZINGELI NA KIBWANA SHOMARI KWA DENIS NKANE SIO MARAFIKI NI NDUGU ZAKE. Denis Nkane mchezaji wa Yanga SC akizungumza na POWER MEDIA amegusia namna ambavyo Maxi Nzingeli ni mtu mwema sana katika maisha yake, na kwake kwa sasa Maxi Nzingeli sio rafiki yake bali kwa sasa Maxi Nzingeli ni ndugu yake. Pia amemtaja Kibwana Shomari, huyu pia ni katika wale wanajeshi wake anaowaamini kwenda nao kwenye vita yoyote ya kimaisha na wakashinda hiyo vita kiufupi huyu ni rafiki yake ambaye wametengeneza mahusiano bora sana ndani na nje ya uwanja. Unajua amewataja nani na nani wengine? Karibu YouTube ya POWER MEDIA ukatazame mahojiano yote