@madiniplus_: Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, anawahamasisha wananchi na wamiliki wa nyumba kubadili mtazamo wa kiuchumi kwa kutumia maeneo yao vizuri zaidi ili kuongeza kipato. Anashauri badala ya kumlipisha mpangaji anayelipa kodi ndogo ya takriban TSh 30,000 kwa mwezi (sawa na TSh 360,000 kwa mwaka), ni bora kutumia eneo hilo kufuga kuku takriban 100 wa kutaga. Anafafanua kuwa kuku hao wanaweza kuingiza hadi TSh 30,000 kwa siku, sawa na TSh 900,000 kwa mwezi au zaidi ya TSh milioni 11 kwa mwaka, na hivyo kumpa mmiliki fursa ya kukuza mtaji na kupanua biashara yake kwa haraka zaidi. Video Mchuchuma TV
Madini Plus
Region: TZ
Tuesday 04 August 2026 10:24:02 GMT
Music
Download
Comments
gracemabula715 :
mhhhh sawa mzee
2026-08-05 09:01:43
0
Mr. JOM :
This man is very smart
2026-08-05 05:26:54
0
Zuli :
gambling 🤣🤣🤣
2026-08-05 07:48:54
0
ambianzi shituka :
biashara nzuri kusimuliwa ingia ndan uwone
2026-08-04 17:16:23
83
Ziggy :
nikwer
2026-08-04 19:28:25
0
Martha Kingu 90 :
haswaaaaaa
2026-08-04 16:39:55
0
Marco Shimiyu :
hizi biashara ni nzuri sanaa kwenye simulizi hivi😂😂
2026-08-04 18:16:16
21
Giantpoultryfarming :
Unachosema Mzee ni sahihi lkn huwezi fuga kuku 100 chumba kimoja. na pia hao kuku wanahitaji uwe na mtaji ili uweze kuwatunza mpk waje kutaga wakuingizie hyo M11 Kwa mwaka. lkn mpangaji haitaji mtaji pia pesa yako ni uhakika unaipokea km ilivyo
2026-08-05 08:00:55
4
THE TRANSPORTER🚘 :
kuku 100 ni million 2 mkuu
2026-08-04 15:52:34
15
lulemuebrania :
taja matumizi na garama zahao kuku acheni kujaza watu mbichimbichi bhana
2026-08-04 12:56:02
11
Dr. Karim :
chakula kwa mwaka anajua kuku wanakula ngapi..? wanatibiwa kwa bei gani, usalama wao wanalindwa kwa bei gani. ukimalkza yoote hayo utajikuta una hasara.
2026-08-04 17:11:32
7
omydulla_01 :
serikali ya kazi na utu
2026-08-05 08:17:51
1
mwelu :
kuku mia wanatosha ukitumia cage tena mpaka kuku 160,sema sasa hao kuku wanahitaji chakula ,dawa pamoja na vitamin ili watage vizuri sana sana hapo wanaweza kutoa faida ya 250,000 mpaka 350,000 kwa mwezi
2026-08-05 07:07:33
1
jaguar one :
Ametoa wazo tuu sio lazima kuifuata
2026-08-04 16:02:50
7
Morgan auto fix :
Fanya wewe tuone
2026-08-04 19:21:56
1
@komanya76 :
mhe mbona kama unawasanua wenye nyumba jaman. uwe na mipaka bas tusje lala nje.😂😂😂😂😂
2026-08-04 20:02:15
2
WAKALI WA MAGARI USED DSM .... :
kideli kwani saiv amna
2026-08-04 19:16:37
1
Dr Luka Mkeni :
sasa mkuu, kuku c wanalishwa,kutibiwa na kulindwa lkn mpangaji huitaji hayo yote
hizo garama umeshazipiga kabla ya kumtoa mpangaji
2026-08-04 11:14:40
21
Saidi Bago :
hayo ni mahesabu yaliyopo tu kwenye maneno twende sasa kwende uhalisia ( vitendo) utaona cha moto 😂😂😂 bro usiamini sana kila unacho sikia kwa influencers
2026-08-05 03:59:47
1
Ashiruna 002 :
Nisaidieni mtaji wa kuku wa mayai 100 ni shs ngapi mpka waanze kutaga
2026-08-04 19:54:23
1
Yao Yao :
Wazo zuri ila hiyo 11ml hupati. labda wote watage na wasife na washibe Mwanga wa jua
2026-08-04 12:56:43
2
kalunde jr :
sasa kuku atakaa kwenye chumba kimoja kaka ?
2026-08-04 17:41:24
1
mtumakin :
sikubalian na ww kiongoz
2026-08-05 06:26:58
1
Jere :
me nina kuku 60 chumba kimoja 2 hawatoshi
2026-08-04 19:15:36
0
RAPH DAVI :
Yaani kiongozi yoyote wa kile chama sijui akipewa mic inakuaje
2026-08-05 07:21:50
1
To see more videos from user @madiniplus_, please go to the Tikwm
homepage.