@newsupdatemedia: Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Jumanne Muliro ametangaza kuanza kwa operesheni maalumu dhidi ya Makundi ya matapeli wanaojihusisha na vitendo vya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, akisema Jeshi la Polisi limetangaza “kiama cha kisheria” dhidi yao. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 4, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Central Police Jijini Dar es salaam, SACP Muliro amesema matapeli hao hutumia mbinu mbalimbali kuwalaghai Wananchi, ikiwemo kujifanya Wafanyabiashara wa madini, Wauzaji wa magari na viwanja, Wanunuzi wa mazao kama korosho na dengu, pamoja na watoa huduma za usafirishaji wa mizigo, kisha kutoweka baada ya kupokea fedha kutoka kwa waathirika. Amesema Jeshi la Polisi limeendelea kupokea malalamiko kutoka maeneo mbalimbali Nchini, yakiwemo Newala, Kibondo, Kasulu na Mbinga kuhusu Wananchi waliopoteza fedha kupitia udanganyifu huo. Kutokana na hali hiyo, Muliro amesema operesheni hiyo itaendelea hadi Watuhumiwa wote watakapobainika na kufikishwa kwenye Vyombo vya Sheria, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vinavyowaumiza wananchi na kuhatarisha usalama wa uchumi. Aidha, ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusu viashiria vya uhalifu ili kusaidia kuzuia na kudhibiti matukio ya kihalifu kabla hayajatokea.#newsupdatemediatz
NEWS UPDATE MEDIA
Region: TZ
Tuesday 04 August 2026 12:16:52 GMT
Music
Download
Comments
TZ 001 :
sisi hatuna ajira tule wapi
2026-08-04 19:12:09
2
DOGO SALU😎 :
kwenye simu usisahau muheshimiwa wanatapeli sanaa
2026-08-04 20:10:25
1
cute2026 :
bila kusahau mawakala tunatapelowa Sana
2026-08-04 21:15:13
1
Erick Erick :
Ongeraaa sana kamanda kwa kazii nzurii🥰
2026-08-05 05:57:18
0
muuh smart driver🇹🇿🇿🇲🇿🇦 :
ongela sana mkuu wa jeshi la police kanda maalumu kwa maamuzi ayo ongela sana mweshimiwa👍👍👍
2026-08-04 16:40:35
0
Nyezuma Issa :
big up Kiongozi
2026-08-05 04:02:30
0
bamsbay wee kam nani unipang% :
apo kwenye viwanjaa matapeli waanauza viwanjaaa badee kuna kua kunashida
2026-08-05 01:25:44
0
Samil Alii :
Jeshi lamaana kabisa
2026-08-04 20:32:43
0
Judy :
siku hizi malipo yote bank ili ushahidi ukuokoe
2026-08-05 05:17:08
0
samwelmasawe :
safi kabisa kamanda
2026-08-04 18:07:20
0
anita :
Kuna utapeli wa wauza simu katika account ya jiji pia Mimi juzi nimetapeliwa simu ya delivery mtu ana account jiji kumbe ni tapeli
2026-08-04 20:52:18
0
Grace mezza♥️ :
Ubarikiwe sana mkuu
2026-08-04 20:02:54
0
Fadhil Omar :
afande kwenye viwanja ndio tunapigwa sana angalia bomoa bomoa ilivyo zagaa dar
2026-08-04 14:46:47
0
user2103355788602neema :
kabisa
2026-08-04 18:30:55
0
Issa Abdallah :
hamuwezi
2026-08-04 19:37:12
0
Ngoshamusic1 :
kuna wengine wanatumia majina ya watu wakubwa kama lugumi wanajifanya wanatoa msaada kwa vijana kuwapa pkpk af wanakuomba pesa ili wakufanyie usajili wa kadi..🥲
2026-08-04 19:23:23
0
Samil Alii :
naaza kulielwa jeshi langu sasa😅
2026-08-04 20:32:25
0
Yordan Yona :
safi sana mkuu hii itokomezwe
2026-08-04 17:08:09
0
NABII CHIDU 🇨🇩 🇿🇲 🇹🇿 :
True
2026-08-04 18:05:16
0
yunnes ❤️🔥 :
bila kusahau walozulumu maisha ya watu 29
2026-08-05 11:22:28
0
seba23 :
naomba namba yako kamba wangu
2026-08-05 11:58:31
0
SR ELECTRICAL AND CCTV CAMERA :
Kweli baba Wapo wengi snaaaa
2026-08-04 17:25:31
0
Abdulsalaam Ghose :
Afande muliro anza na uyo muhindi apo central police anaitwa shabbir Mohamed somji afande George deputy ananjua
2026-08-04 17:50:36
0
BUILDING SOLUTION :
Hii ndio kazi sasa ya Jeshi la Polisi..walinzi wa Raia na Mali zake...twende Kazi...
Boss kwezi umefikiwa😂😂😂😂
2026-08-04 15:53:15
1
To see more videos from user @newsupdatemedia, please go to the Tikwm
homepage.