abdulmaliki salafii :
Assalamu 'alaykunna warahmatullahi wabarakatuh, dada zetu Waislamu.
Tunawakumbusha kwa upendo kwa ajili ya Allah. Mcheni Mwenyezi Mungu katika siri na dhahiri, kwani dunia ni ya kupita na Akhera ndiyo makazi ya milele. Linda Swala tano kwa wakati wake, shikamaneni na Qur'an na Sunnah, zidisheni dhikri, dua na kutafuta elimu yenye manufaa.
Jilindeni na maasi ya wazi na ya siri, hususan yale yanayofanywa kupitia mitandao ya kijamii. Kila neno, picha na kitendo kinaandikwa, na siku moja tutasimama mbele ya Allah kuhesabiwa. Tubu kabla mauti hayajafika, kwani hakuna anayejua siku yake ya mwisho.
Chagueni marafiki wema wanaowakumbusha Allah, vaeni kwa staha, dumisheni haya na tabia njema, na msikubali dunia au sifa za watu ziwatoe kwenye njia ya haki.
Kumbukeni kwamba uzuri wa kweli ni uzuri wa imani, uchamungu na tabia njema. Tunamuomba Allah Awalinde, Awasamehe madhambi yenu, Awaimarishe katika dini Yake
2026-08-05 22:19:24