@bongofive: Peter Okoye (Mr P) azidi kufichua yaliyotokea ndani ya familia ya P-Square, Msanii huyo ameendelea kuelezea kile kilitokea mwaka 2015 katika mgogoro wa kifamilia kati yake, ndugu yake pacha Paul Okoye (Rudeboy) na kaka yao Jude Okoye, ambaye alikuwa msimamizi wa kundi hilo. Katika maelezo yake, Mr P pia amedai kuwa kipindi hicho kulikuwa na tukio ambalo alihisi usalama wake ulikuwa hatarini, akieleza madai ya kutishiwa maisha na Jude Okoye wakati wa mvutano huo wa kifamilia. Baada ya Peter Okoye kuendelea kueleza upande wake kuhusu mgogoro wa kifamilia na masuala ya biashara ya muziki, sasa Jude Okoye amejitokeza hadharani kujibu madai hayo, akisema baadhi ya maelezo yaliyotolewa na Peter si ya kweli na kuonesha baadhi ya vithibitisho. 🎤……. @cathed__