@chellaboywiz: Ukweli mchungu: Kila biashara ina FAIDA na HASARA (hilo liko wazi). Lakini hakuna mjasiriamali mwenye akili anayeamka asubuhi, akatoa mtaji wake, kisha akaanza kupanga mikakati ya "jinsi ya kupata hasara". Lengo namba moja siku zote ni kutengeneza FAIDA! Hasara ni matokeo ya mfumo kufeli. Kuna watu wanalalamika kwenye comments wakisema tunaongelea sana faida kana kwamba tunauza 'utapeli', na kwanini hatuongelei hasara. Sikiliza, kama unaanza biashara ukiwaza hasara, tayari umeshafeli kisaikolojia. Biashara ni mchezo wa kuchukua hatari (Taking Risks) na kujaribu mifumo mipya mpaka itikise soko. Kama unaogopa hasara asilimia 100, biashara haikufai, tafuta ajira! Kwenye hii page hatufundishi uoga, tunafundisha MIFUMO ya kupunguza hasara na kumaximize faida. Wanaoelewa somo wapo bize kuchukua madini na kuingiza hela, wanaoogopa wataendelea kupinga kwenye comments! 🧠 🧠
Chella_Boy_Wiz🤟🤟🤟
Region: TZ
Tuesday 04 August 2026 17:48:33 GMT
Music
Download
Comments
spark :
awo vijana waaminifu sas pakuwapata
2026-08-05 14:29:42
2
Stella msphe :
imekaa kitaalam sana
2026-08-05 12:18:23
2
dally veer :
kati ya watu wanne nliwafollow wewe n miongon nwao 😂,,, hongera sana unajua
2026-08-05 08:35:35
3
JUNIOR GIDEON :
vip kuusu mtaji na upikaji
2026-08-05 11:56:10
0
𝐄𝐦𝐬𝐚𝐦𝐏𝚛𝚘 :
biashara msiwe mnaziweka Kwenye calculator fanyeni vitendo
2026-08-04 18:27:44
0
Materu Don :
embu anza tuone
2026-08-05 06:37:16
1
FEMILUX NAILS 💅 :
Biashara ya kupakaa kucha rangi embu ongerea
2026-08-04 19:08:12
1
Chiriku1 :
yaaan uuze kachori z
2026-08-04 18:33:04
1
official Elia :
🔥🔥
2026-08-04 18:28:17
1
Manager :
😁😁😁
2026-08-05 11:57:43
1
To see more videos from user @chellaboywiz, please go to the Tikwm
homepage.