@jwtz80: Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali lbrahim Mhona, amewataka wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Mdogo kuhakikisha wanaendelea kufanya Mafunzo ya kijeshi katika vikosi vyao ili kujiweka tayari kutekeleza majukumu yaliyo mbele yao wakati wowote. Meja Jenerali Mhona amesema hayo leo Juni 12, 2026 wakati akihitimisha kozi ya Uongozi Mdogo Kundi la 15/2026 iliyofanyika katika kikosi cha JKT Mafinga mkoani Iringa, kwa usimamizi wa Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa ( CUJKT), kilichopo Kimbiji jijini Dar es Salaam. #jeshilakujengataifa #lindataifalako