MWAKANYAMALE :
🎚️MKRISTO, UKISHAONA TU MTUMISHI ANAONGELEA WATU BADALA YA NENO KIMBIA! ANAONGEA SANA MANENO BADALA YA NENO KIMBIA! ANAONGEA VITU KUKUSIFIA TU UJUE ANAKUTEKA UFAHAMU KIMBIA! ANAONGEA MAMBO UNAYOYAPENDA SI MUNGU ANAYOPENDA, KIMBIA! UAMUZI NI WAKO, KUANGAMIA NI KWAKO HULAZIMISHIWI UNAKUMBUSHWA!
-Ibilisi anacheza na akili yako Mkristo yale mwili wako unayopenda. Madhehebu yote yanayomuabudu Mungu aliye hai katika Kristo Yesu ni mazuri mbele za Mungu, shetani ndiye mbaya, sikiliza kwa makini unayoambiwa na uwe makini unayemsikiliza usisikilize maneno sikiliza neno, watu wengi wanapenda kusifiwa ndio mbinu inayotumika hapo, haijalishi mtu anakusifia pima anachokwambia kipime na neno! Biblia inasema "shetani asije akapata kuwashinda kwa sababu hamkosi kuzijua fikra zake." ZABURI 1:1 "Heri mtu asiyekwenda katika shauri la wasio haki."
-Mungu ameagiza uzivae silaha zake zote ili uweze kuzipinga hila za shetani, moja ya hizo silaha ni Upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu, wengi hawanana neno nani yao hivyo ibilisi anawatumia wajumbe wake kuwapepeta kama ngano ili imani yao ipungue. Ninakuombea kisiwepo cha kukutenga na Mungu kama ilivyoandikwa kwenye WARUMI 8. Uamuzi ni wako usimame imara kwenye imani au usikilize maagizo ya wandamu, wadanganyifu wamemwagwa wengi na watapotosha wengi Biblia inasema usipokuwa makini hata waamini watapotoshwa, Mungu hana hasara ukipotea atachukia ukifa dhambini lakini unayekufa dhambini ni wewe Mungu hafi Yuko hai, utakayekwenda motoni ni wewe Mungu hahusiki! Pima Mtumishi unyemsikiliza kama haongelei kuhusu siku za mwisho, masuala ya kuacha dhambi, haongelei utakatifu ujue haendi mbinguni!
2026-08-09 15:42:20