@emanuel_walwa: Kama haupo tayari kuweka uwepo wako 100% kwenye biashara yako mwanzo, tayari umeshafeli kabla hata hujaanza! 🚨 Watu wengi wanaanza biashara wakifikiri ni njia rahisi ya kuongeza kipato cha pembeni au kuziba pengo la ajira. Ukweli mchungu ni kwamba: Kwenye hatua za mwanzo, WEWE ndio mfumo, na WEWE ndio maono. Kujiajiri kunatofautiana sana na kuendesha biashara inayojitegemea. Ukijidanganya kuwa biashara itajiendesha yenyewe bila usimamizi wako, unapoteza mtaji wako. 💡 Unakubaliana na wazo hili au una mtazamo tofauti? Dondosha maoni yako hapo chini! 👇 📌 Hifadhi (Save) post hii ukumbuke kila unapotaka kuanzisha mradi mpya. 📲 Mtag mjasiriamali au rafiki yako anayepanga kuanzisha biashara hivi karibuni! #Biashara #ElimuYaFedha #Ujasiriamali
Kaka Emma, sometimes tunafanya biashara ili end of the day tuwe na freedom na sio kuwa busy as employee.... but namuelewa sana mtoa mada in some angles
2026-08-10 06:23:30
1
mziwander_store :
Mimi nisipo kuwepo dukani kwangu mauzo. Yanashuka. Ko ndo maana mm nipo mwenyewe 😂😂😂
2026-08-09 08:24:02
27
kelvin_Mveti :
Kma biashara yako haiendi ukiwa haupo hiyo sio biashara ni Ajira😅
2026-08-08 17:22:26
57
Issa :
Free Juma Jux
2026-08-10 01:05:44
4
mussamashishanga :
Utamaduni wa biasshara yako unaweza kuifanya ikue, iifanye vizuri. hata kama haupo...anachokkielleza huyo bwana ni business trap kwa mmiiliki wa biiashara.
2026-08-09 19:19:17
1
JITU LA MBINGUNI :
niuze nyumba nifanye biashara
2026-08-09 08:38:19
1
G+255🇹🇿🇹🇿 :
huo ndio ukwel
2026-08-08 16:17:16
3
victor william :
sijui nifanyeje
2026-08-09 10:41:25
1
deorgatius :
🤣🤣🤣 mzee anaye bisha na abishe Ila mzee kasema ukweli mtup
2026-08-09 17:06:09
8
Magreth fashion store :
Daaaah wengine tunakuwa kazin kutafuta mtaji sasa me nmefungua biashara na sina mda huko natafuta mfanyakz nfanyaje naomha ushaur
2026-08-08 18:07:54
5
synaGive :
wekeni kamera wafanya kazi wanaogopa ila sio Mimi kuiba kidogo kawaida hiyo
2026-08-09 21:44:49
1
Deolee Lucas :
afu biashara haipo ivo we kaka unaavozan ayo maneno nitofauti na unachokisema
2026-08-09 19:51:01
1
deby :
yaan mm hata nikiugua tu najikokota hivohivo kwenda maana nikifunga nakosa amani kabisa😅
2026-08-09 11:02:03
1
ulukuwaimjukuu :
Yaani mimi kila mara nakula mwereka😭😭sipati wafanyakazi wazuri
2026-08-09 08:57:53
6
MUTE.COM :
We Kabenda ulikuwa umeenda wap jamn? mimi naktafta sana siku hizi ulikuwa umepotea mtandaoni aisee,tumemic madini yako
2026-08-09 07:27:24
1
ibrahimmistaazam :
washauri mnatuchanganya mnasema tusiache kaz lkn tuwe na vyanzo sasa tutajigawa vp
2026-08-09 10:00:13
1
Magreth fashion store :
Sio tamaaaa ukikosa kazin unapata kwenye biashara
2026-08-08 18:08:33
3
Manuel@🍁 :
washauri mmekua wengi sana tatzo ni usimamizi na biashara ipi Kuna ambazo zinasimamika ata ukiwa haupo
2026-08-09 06:40:37
1
AFYA YA UZAZI YA MWANAUME001 :
vipi kama ni mtaa wako hapohapo
2026-08-09 12:54:13
1
YouTube @Nitume Mimi Ministry :
biashara nzuri/au uwekezaji mzuri ni pale hata haupo biashara inasonga mbele,, lakini biashara mpaka uwepo umeikodolea macho hapo naona siyo
2026-08-08 17:43:51
3
Omasala :
sio kweli, labda tusema kwamba wakati mwingine tunafeli kwa kukosa kuijua vyema biashara uitakayo au uianzishayo, unaweza ukaanzisha biashara na ukaipa minimal supervision huku ukiendelea na kazi au biashara nyingine, mfano ninao watu wengi ambao ni wafanyakazi ila wamefungua biashara moja na baadae wakafungua branches hata nje ya mikoa wanayoishi, kuna vitu vya kuzingatia ili kuanzisha biashara hata kama ukiwepo na hujafuata misingi hiyo, utafeli tu, tukikybali hilo tutaua mawazo ya kujiajiri wakiwa kazini.
2026-08-08 18:33:29
2
Chongera Yahaya :
aisee hiyo nisawa broo
2026-08-08 18:49:03
2
Bahati Leonady :
kwann ufel
2026-08-08 18:38:36
2
Ankali Movies :
asante
2026-08-09 07:47:34
2
To see more videos from user @emanuel_walwa, please go to the Tikwm
homepage.