@abdalla.basawad: DAY TWO; Baada ya zoezi la uwezeshaji wa wafanyabiashara wadogo kupitia BASAWAD PAWA FOUNDATION, tumepata fursa ya kusikiliza maoni na hisia zao kuhusu athari za programu hii. Maoni yao yametupa nguvu na hamasa ya kuendelea kubuni na kutekeleza mipango inayoinua uchumi wa wananchi wetu. Tunathamini kila ushauri, pongezi na mapendekezo yaliyotolewa, kwani ndiyo msingi wa kuboresha huduma zetu na kuhakikisha kuwa uwezeshaji unaleta matokeo chanya na ya kudumu. Kwa pamoja, tunaendelea kujenga jamii yenye biashara imara, familia zenye kipato, na maisha bora kwa wote. #MJAMBEREPAWA.