@wepesitv: Hali ya taharuki imewakumbuka wakazi wa kijiji cha dareda kati kata ya Ayagalaya Wilayani Babati mkoani Manyara ambapo mtoto mchanga mwenye jinsia ya kike ameibiwa na watu waliojitambulisha kama wauguzi katika kituo cha afya cha Dareda kati ambapo tukio hilo linadaiwa kutokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia Jumapili Agosti 9, 2026. Wauguzi feki hao walisema wanamchukua mtoto huyo kwaajili ya kwenda kumpatia chanjo kwa majira hayo lakini hawakuweza kurejea tena ndipo mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye rahma mpinga alipokutwa na wasi wasi na kuanza kufuatilia suala hilo bila mafanikio yoyote yale, Familia ya Rahma Mpinga wameelezea tukio zima jinsi lilivyo tokea huku wakielezea namna watu hao walivyo wasili na kumchukua mtoto huyo ambapo watu hao inadaiwa walikuja na usafiri wa gari aina ya noah kisha kutokemea na mtoto huyo, aidha wameiomba serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaidia kumpata mtoto huyo kwani ni tukio la kuhuzunisha katika familia yao, Kwa upande wake Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Madama Hosea amekiri kutokra kwa tukio hilo huku akielezea namna ambavyo hatua za awali zilivyo chukuliwa ikiwemo kuwasiliana na jeshi la polisi lakini pia ameelezea namna ambavyo utaratibu wa kutoa huduma za chanjo katika kituo hicho haupo katika majira ya usiku hivyo watu hao hawakuwa waauguzi wa kituo hicho lakini pia amesema wauguzi wa kituo hicho wanafahamika kwa sare zao na taratibu zilizowekwa katika kituo hicho Aidha, Kaiumu mkuu wa Wilaya ya Babati Remidius Mwema akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama amefika katika kituo hicho na kuangazia namna ambavyo tukio hilo limetokea kisha kutoa maelekezo ya serikali kwa ujumla pamoja na kuelezea namna ambavyo hatua za awali zilivyo chukuliwa.