@doctor.lucky14: Gingivitis au ugonjwa wa fizi kutokana na bakteria. Meno kuwa na tartar/calculus, ambayo haiwezi kuondolewa vizuri kwa mswaki pekee. Kusafisha meno kwa nguvu sana au kutumia mswaki mgumu. Chakula kubaki katikati ya meno. Meno kuoza au kuwa na maambukizi. Mabadiliko ya homoni, mfano wakati wa ujauzito au hedhi. Kisukari au hali nyingine zinazopunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi. Upungufu wa baadhi ya virutubisho, hasa vitamin C. Uvutaji wa sigara. Baadhi ya dawa zinaweza pia kusababisha fizi kuvimba. #meno #afya #matibabu #doctorprossy