@sautitv9online: zilizopitaLissu amuhoji shahidi kama alipewa jina la mwanachadema yeyote aliyekua hatarini kwa vitisho Lissu: Waeleze majaji kama uliwasilisha hiyo barua Shahidi: Ipo Lissu: Ipo Mahakamani Jajji: Shahdi embu jibu kama umeleta au hujaleta mawakili wa serikali watakuuliza baadae pia Lissu: Kwa hiyo jibu ni lipi Shahidi: Sijaleta Lissu: Nataka maswali yangu yajibiwe kwemye ushahidi wako, jana ulisema hivi baada ya kaungalia hiyo video uliona kwamba mtuhumiwa alidhihirisha nia yake kwa kuchapisha kwa umma, kwa kuchapisha kwemye Jambo TV. Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako Shahidi: Hayapo Lissu: Shahidi kwenye ushahidi wako kuhusu tuhuma ulisema, uchaguzi mkuu uko kwa mujibu wa Katiba na mlinzi mkuu wa Katiba ni serikali. Umewahi kusoma Katiba? Shahidi: Kipindi cha nyuma Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimsomee Katiba, Ibara ya 26 - "Kila mtu ana wajibu wa kulinda na kuzifuata na sheria za nchi hii, wewe umesema ni serikali Shahidi:....... Lissu: Ulisema kulikuwa na mipango ya kuvuruga uchaguzi kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kupiga watu mawe na mengineyo, waeleze majaji kama hayo maneno yako kwenye maelezo yako Shahidi: Hayapo Lissu: Jana ulisema hivi, hiyo video mliyoiangalia iliwekwa kwenye 'memori kadi' ikafikishwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi ili kuithibitisha, sasa waeleze majaji kama hayo yapo kwemye maelezo yako Shahidi: Hayapo Lissu: Kwa kuwa wewe ni shahidi wa 16 na wengine 15 waliopita hawakuwasilisha video Mahakamani naomba waeleze majaji kama umewasilisha hiyo video Shahidi: Hapana Lissu: Kwakuwa wewe ni shahidi wa 16 na hakuna aliyewasilisha ripoti ya kubaini uhalisia wa hizo video, waeleze majaji kama umewasilisha hiyo ripoti ya uchunguzi Shahidi: Hapana Lissu: Unasema ulimuelekeza Inspekta Michael kuchukua vielelezo pamoja na ripoti ya uchunguzi na kukabidhiwa kwa mtunza nyaraka. Je, hayo yapo kwenye maelezo yako? Shahidi: Hayapo Lissu: Baada ya kufanya yote ambayo mlikua mmeshafanya uliwasiliana na Ma RCO nchi nzima, hiyo ipo sitakuuliza, sasa kwenye maelezo yako jana umetaja majalada ya uchunguzi toka mikoa mbalimbali; Ruvuma, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam. Mimi nakuuliza juu ya jalada la Dar es Salaam, toka ofisi ya ZCO ambalo namba zake ni….. waeleze majaji kama lipo kwenye maelezo yako. Shahdii: Hayapo Lissu: Jana ulisema mtuhumiwa alikamatwa Mbinga na kusafirishwa usiku huo huo mpaka Dar es Salaam, Kituo Kikuu cha Kati na kufikishwa ofisi ya Deputy ZCO. Waeleze majaji kama hapo maelezo Shahidi: Hayapo Lissu: Ulieleza pia jinsi ulivyopeleka jalada ofisi ya DPP na baadae jalada kurejeshwa kwenu kuendelea na upelelezi, waeleze majaji kama hicho kipande kipo Shahidi: Hakipo Lissu: Unasema mlipata taarifa mashahidi kutishiwa, je kwemye maelezo yapo? Shahdi: Hayapo Lissu: Unasema mliwasiliana na ofisi ya DPP ili kuweza kuwapatia ulinzi mashahidi, Je yapo? Shahdi: Yapo Lissu: Unasema mliomba kwa barua sema kama yapo Shahidi: hayapo Lissu: Unasema ulikula kiapo ili kuwaombea ushahidi, Je yapo? Shahidi: Hayapo Lissu: Hayo ni kutoka kwenye ushahidi wako jana sasa twende kwingine, umewaeleza majaji kwamba umesoma hiyo hati ya kiapo? Shahidi: Ndio Lissu: Waeleze majaji kwenye hati hii uliyosaini kama ulitaja jina la shahidi yeyote Shahdi: Hapana Lissu: Waleze majaji kama ulipewa jina la mwanachadema yeoyote aliyekua hatarini kwa vitisho Shahidi: Hapana Lissu: Waleze majaji kama ulitaja mwanachama yeyote alikua akitoa vitisho hivyo Shahidi: Hapana Lissu: Waleze majaji kama ulitaja siku au mahali Shahidi: Hapana Lissu: Waeleze majaji kama ulitaja aina ya vitisho Shahidi: Ndio nilitaja Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimuoneshe shahidi kiapo chake

𝗦𝗮𝘂𝘁𝗶 𝗧𝘃9 𝗢𝗻𝗹𝗶𝗻𝗲
𝗦𝗮𝘂𝘁𝗶 𝗧𝘃9 𝗢𝗻𝗹𝗶𝗻𝗲
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 11 August 2026 09:02:56 GMT
56368
920
29
22

Music

Download

Comments

likiiboympole
Øfficially likiibøy Mpøle✌️🎬 :
man of judge👨‍⚖️👨‍⚖️👨‍⚖️✌️✌️✌️
2026-08-11 09:14:51
1
siraji.mbaba
Siraji Mbaba :
i.love u lisu
2026-08-11 10:52:39
0
alexkasuga8
alexkasuga8 :
Jesus power
2026-08-11 15:08:30
0
jikwaka7
JIKWAKA :
Lisu ahsante kwayote endelea kutoa elimu naami hakuna asiye jifunza kwako mpaka dakika hii tunakusubiri uraiani.
2026-08-11 13:02:53
7
anambwesanga
Anambwe Sanga :
Mmmmmmm
2026-08-11 14:08:35
0
jabalila.tz
JABALI la Tz :
School of law Kuna kitu Cha kujifunza kwenye hiii kesi...🤔
2026-08-11 10:45:55
6
jbmweofpiw4
jbmweofpiw4 :
lisu madai ns ushahidi wa Kutengeneza unakukomaza ktk kutoa maamuzi.
2026-08-11 12:25:45
3
user7314619976016
user7314619976016 :
tunakupenda lisu
2026-08-11 11:51:41
0
fm4482
FM :
kweny hii kesi mawakili wanaojifunza waalikwe kama internship yao
2026-08-11 15:53:40
0
keraryo.mwita
Keraryo Mwita :
Kuna watu na mtu
2026-08-11 14:50:50
0
rose.tika71
Rose Tika :
Viva Lissu
2026-08-11 13:46:36
0
abelymwalukali
Abely Mwalukali :
tutafika tu tunapotaka kwenda
2026-08-11 13:22:26
0
japheti.alleny
Japheti Alleny :
bigapu sana ndugu lisu tupi pamoja kwene maondi
2026-08-11 12:44:48
1
frank.mkristo
Frank Mkristo :
kuna mwisho kwenye kila jambo ,
2026-08-11 13:13:05
0
shax7503
Shax :
baba wa taifa
2026-08-11 09:46:38
1
user47266941046922
user47266941046922 :
Mungu atawatesa watesi wako ck 1
2026-08-11 11:52:12
0
tomkamau64
Tom Kamau :
Pongezi Mhe Tundu Lissu..unaendelea vizuri kwa utulivu ulio kamilika. Twaomba Mungu akujalie neema na ujuzi wa kutosha ...na afya na amani. Yote haya yatapita hivi karibuni..Mungu pamoja nasi . Kutoka Nbi, Kenya
2026-08-11 12:26:53
0
abasi.ahmadi
Abasi Ahmadi :
mungu akujalie mwishimiwa wetu utoke kwnye mtiani hu tunakupenda san kumbuka Ata Nelson Mandera aliyapitia magumu km yako ila alikuja kuitawala sauthi mungu yupo pamoja na wew
2026-08-11 09:32:38
15
mr.gbles
Mr Gbless18 :
Naomba, wanafunzi wote mnao somea sheria,. Ili kutoa haki za kisheria mjifunze kitu kupitia,. MH : Tundu lissu. Na nataka awe analipwa hata asipo achiliwa. Na akitoka akabiziwe kuwa mkufunzi mkuu wa vyuo vya sheria... 😂 DPP naomba lissu aendelee kubaki ndani. Ili tuendelee kujifunza sheria kupitia kesi yake ya uhaini.. 🙏🫡🫡 #Free Tundu antipas Lissu🙌
2026-08-11 14:21:24
2
user7949456748181
user7949456748181 :
ivi udhaifu huu hawezi kustua watu nakufuta kesi ili wasiaibike zaidi
2026-08-11 13:35:46
0
officialafrican.tz
AfricanTz :
je akifa Andiko alitatimia?
2026-08-11 14:35:50
0
swagz1234tz
KISWAGA FREDY :
Hili kichwa napenda mwanangu mmoja afikie uwezo huu .... mbona mahakama zinaenjoy na kesi 🥰
2026-08-11 15:02:19
0
mmarodennis.munuo
Mmaro-DENNIS MUNUO :
Congratulations Lisu for the Power, Wisdom and strength given by God the Father, There is a Commandment in the Bible that says, Again it is God who said, Do not bear false witness against your neighbor, That is the Commandment of God Himself, Remember Nyie Mashahidi,Utakuja kusimama Mwenyewe kwenye Maisha yako na familia yako,Utakuja kujuta,sik
2026-08-11 13:10:36
0
son.of.habakuki
son of habakuki :
unaweza kimbia maswali heee
2026-08-11 12:57:04
0
ifabby23
TANGO ONE :
shahidi anaona moto sanaa😂😂😂😂😂😂
2026-08-11 12:51:20
0
To see more videos from user @sautitv9online, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About