@chawamata_tv: VIDEO: Madereva watano wamekamatwa katika operesheni iliyofanywa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani katika maeneo ya VETA na Mnazi Mmoja mkoani Lindi, kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujiongezea madaraja ya leseni bila kuwa na sifa stahiki. Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, Afisa wa Polisi kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Rutusyo Hakimu Mwambelo, amesema katika operesheni hiyo madereva wawili walikamatwa katika eneo la VETA baada ya kubainika kuwa na leseni za daraja D, lakini walikuwa wamejiongezea daraja E kinyume cha taratibu. Amesema baada ya kuhojiwa, madereva hao walibainika kuwa hawakuwa wamekwenda darasani kusomea daraja hilo, bali walikuwa wakitoa fedha na kupewa vyeti, jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Aidha, katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi, madereva wengine watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kughushi vyeti vya vyuo pamoja na kujiongezea madaraja ya leseni ambayo hawana sifa ya kuyaendesha. Madereva hao wamewekwa chini ya ulinzi huku taratibu nyingine za kisheria zikiendelea. Mwambelo amewapongeza madereva wa mabasi wanaozingatia sheria na taratibu za usalama barabarani, akisema madereva wengi waliokaguliwa wamekuwa na leseni halali pamoja na nyaraka nyingine muhimu. Aidha, amesema Jeshi la Polisi limetoa elimu kwa madereva na abiria kuhusu usalama barabarani, hususan umuhimu wa abiria kufunga mikanda, akieleza kuwa hatua hiyo inaweza kupunguza madhara wakati gari linapopata ajali au kuyumba baada ya kukutana na mashimo barabarani. Amewataka madereva ambao hawajasoma vyuoni lakini wamejiongezea madaraja ya leseni kuacha kutumia njia za mkato na kwenda kupata mafunzo rasmi, akisisitiza kuwa hawapaswi kusubiri hadi wakamatwe ndipo sheria ichukue mkondo wake, kwa kuwa kughushi nyaraka ni kosa kubwa kisheria. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #MediaTanzania #OnlineTV #TrendingTZ #TanzaniaTrending #ViralTZ #TeamChawamata #SupportLocal #madeintanzania🇹🇿 #madeintanzania🇹🇿 #madeintanzan #madeintanzania #SupportLocal #madeintanzaniat #roadto100followersontwitch #madeintanzaniawith #viraltz
CHAWAMATA TV
Region: TZ
Tuesday 11 August 2026 09:45:51 GMT
Music
Download
Comments
KESSYSINGE Lizaboni :
safisana
2026-08-11 10:59:03
0
fabiani emmanuel :
yaani hiii inchi ivi mnajua madhara mnayo yatengeneza lkn ivi kila siku nyie ni madereva ...ivi mnajua ni jinsi gani mnatesa familia zetu yan mtu ameendesha lori miaka kumi na nane una mtoa kqzin akafundishwe nin ...em acheni watu wafanye kaz kwann kila cku mnatunyanyasa..tumewakosea nn nyie...nyie toka mme ajiliwa nilini mlirud chuo kufundishwa upya .
2026-08-11 16:57:24
23
Minister transporter dodoma :
kazi ya udereva ishakuwa ngumu wanatuwaza sana awa watu
2026-08-11 10:59:54
43
Nzore boy :
Kuna sheria zinapaswa kulinda maisha ya watu, lakini pia kuna sheria ambazo zinahitaji kuangaliwa upya ili ziendane na maisha halisi ya wananchi.
Miaka mitatu kusubiri kuongeza daraja la leseni ni muda mrefu kwa mtu ambaye tayari ana uzoefu, ana uwezo na ana familia inayomtegemea. Usisahau kwamba nyuma ya dereva mmoja kuna familia, watoto na watu wengi wanaotegemea kipato chake.
Tukiweka masharti magumu kupita kiasi, tusishangae kuona baadhi ya watu wakitafuta njia za mkato na kuishia kwenye uhalifu wa kufoji leseni. Badala ya kusubiri tatizo litokee, tuweke mfumo unaowezesha mtu mwenye uwezo na sifa kuongeza daraja lake kwa njia halali, salama na yenye uwajibikaji.
Sheria ziwe na lengo la kulinda maisha, lakini zisije zikawa kikwazo cha maisha ya wananchi. Tupunguze masharti yasiyo ya lazima, tuongeze uwajibikaji na tuwape watu wenye uwezo nafasi ya kusonga mbele.
2026-08-11 21:01:33
3
temba :
ivi mbona sijawai kuskia dereva wa serekali kakamatwa kwaajili yamambo kama haya au hao niwakamilifu
2026-08-11 10:58:07
13
MWANAMONSI💪 :
kwa iyo kama hawana taaluma.izo gari wamewezaje? kuendesha
2026-08-11 11:16:48
9
Mubah brown :
ila mnatukosea sana me lesen yang imeisha nataka sasa nikasome wamesema hawapokei lesen zilizoisha sas hapo nifanyaje apo
2026-08-11 11:03:47
11
muhsini :
kwani leceni inatokea wapi hiinchi Yani dah nachoka
2026-08-11 10:42:03
8
Ibrahim Temba :
wanatoa hela kwa nani?
2026-08-11 18:05:06
1
CHIDY LOVE :
HII NCHI UKIIBA MABILION YA PESA UTABADILISHWA KITENGO ILA UKIIBA KUKU JELA MIAKA 6 AU FAIN NDO HII
2026-08-11 17:57:28
3
mamu :
mnatucheleweshea reseni tunasoma tunakaa miezi mingi bila kazi tupeni reseni mnatupanga mnataka tuishije?
2026-08-11 17:00:00
3
husseinmanangwa :
waliopitisha hizo lesen mmewachukulia hatua gan? maana chanzo cha makosa yameanzia hapo. lesen MTU awezi jiongezea bali ni hao hao. wanaongeza.
2026-08-11 13:02:17
7
joshua JS :
mbona hii serikali wanakazana sana madereva
2026-08-11 14:05:17
2
acheni watu wapate rizikhi ukimuweka ndani na anafamilia mnatengeza nini kama sio laaana vipi ingekuwa wewe ni mama na unamtegemea uyo mtoto dereva afu unasikia kawekwa ndani tumieni busara na si nguvu
2026-08-11 11:04:42
9
Mr KIGOMA :
kkubwa tuu sahv game kwny swal la udereva n gum saana, kam vp madereva wote tugome tuuu mamb yasmame
2026-08-11 18:30:52
0
Fela :
mnaacha kwenda kukamata waharifu mnahangaika na madereva wenye uzoefu wa hizo kazi iii nnchi nachoka kabisa
2026-08-11 21:30:35
1
senzo.xo :
waliopitisha hizo lesen mmewachukulia hatua gan?
2026-08-11 10:18:17
6
Wabusara :
HAO WALIO IZINISHA HIZO LESENI SI WANAFAHAMIKA TRA POLISI SASA HIZO LESENI WAO WAMEZIONGEZAJE LABDA TUFAFANULIENI
2026-08-11 15:23:22
0
👑 KiBELLa oG :
SAFII KUNA WATU WANAWAWEKEA UGUMU WENZAO KATIKA KAZI
2026-08-11 10:24:44
0
Clemence Temu :
kumeanza kuchangamka
2026-08-11 10:43:25
0
Contawa OG :
tupo wengi tupo wengi
2026-08-11 16:05:48
2
Dulla2410 :
Kusukuma gari sio kazi Bali kazi ni kuzijuwa sheria za barabarani ajali ni nyingi tuacheni ukaidi tukasomee 🔥
2026-08-11 14:58:00
1
J king👑 :
madereva tusomenitu kwani tumeshika kwenye Makari wao wameshi mipini madereva tumasomeni Sheria nizirezire tukasome tuondokane namizozo barabarani🙏👍
2026-08-11 15:35:55
1
ngosha OG :
kuna kitu nataka kucomment jambo ila basi
2026-08-11 10:33:00
2
Dento__tz :
Mtu ameendesha gari niaka 10 unapeleka darasani kufanya nn?acheni watu wafanye kazi
2026-08-11 14:42:10
1
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm
homepage.