@tcra_tanzania: Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb.) amesisitiza umuhimu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu, kuripoti majaribio ya ulaghai kupitia namba 15040. Mhe. Kairuki amesisitiza hayo wakati akiwasilisha ripoti ya hali ya Sekta ya Mawasiliano kwa robo mwaka iliyoishia Juni 2026, kwa waandishi wa habari, tarere 10 Agosti, 2026 katika ofisi za Makao Makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam. Ripoti hiyo inaonesha kupungua kwa majaribio ya ulaghai mitandaoni kwa asilimia 25.29 hadi kufikia mwezi Juni 2026, ikilinganishwa na ilivyokuwa mwezi Machi. Tembelea tovuti ya TCRA kupitia www.tcra.go.tz kupata ripoti kamili au fungua kiunganisho hiki https://bit.ly/4z2K84t au skani kodi ya QR iliyopo kwenye bango. NMUHIMU 📌Mawasiliano baina ya mtoa huduma na mtumiaji wa huduma za mawasiliano ni kupitia namba 100 pekee; 📌 Ripoti majaribio ya utapeli kupitia namba 15040 (tuma namba ya aliyekupigia au kukutumia ujumbe wa kitapeli); 📌 Hakiki laini zilizosajiliwa na NIDA yako kwa kubofya *106# #tcratz #statistics #sektayamawasilianotz

Mamlaka ya Mawasiliano 🇹🇿
Mamlaka ya Mawasiliano 🇹🇿
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 11 August 2026 13:04:59 GMT
2265
50
4
12

Music

Download

Comments

ukerewe0
UKEREWE🇹🇿 :
tunaomba pia simu zinazoibiwa tuwe tunatoa taarifa kwenu kwa kutuma imel ya simu na email na namba ya simu ya muhusika wa alieibiwa itapendeza sana
2026-08-15 18:04:14
0
sifadesigner
@sifa_designer :
Tunatoa taarifa hakuna feedback! Mwenyewe nimeacha kutoa
2026-08-14 13:52:55
0
mr.desert2025
MRDT :
hiyo namba haikati pesa?
2026-08-14 10:12:21
0
victoria.gl20
Victoria GL :
vipi zile simu tunazonyakuliwa buguruni na jangwani ni kweli tcra hawaiwezi kuzitruck? ni kweli polisi wameshindwa kuwakamata hao wezi?
2026-08-12 05:56:30
0
To see more videos from user @tcra_tanzania, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About