@uhondo.tv: Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) jana Ikulu. Akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Kilosa Mjini, mkoani Morogoro, Hapi amewataka Maaskofu hao kuwaombea viongozi wa CHADEMA ili waondokane na pepo ya ukaidi na kuitikia wito wa kwenda kwenye meza ya maridhiano. Hapi amesema Rais amekuwa akitoa nafasi kwa vyama vya siasa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala ya Taifa, lakini CHADEMA hawajaitikia wito huo. Amesema TEC imeonyesha mfano kwa kuitikia mwaliko wa Rais na kukutana naye, hivyo amewaomba Maaskofu kutumia nafasi yao kuwaombea viongozi wa CHADEMA ili nao wafunguke na kuona umuhimu wa mazungumzo. “Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA. Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi. #UhondoTVUPDATES
Uhondo TV
Region: TZ
Tuesday 11 August 2026 14:12:00 GMT
Music
Download
Comments
alice :
Ivi maridhiano bira chadema aiwezekani
2026-08-11 15:15:42
0
the man of the people :
hatuendiii,hata siku moja
2026-08-11 15:20:32
0
jupter :
akuna kwenda fanyeni malidhiano na hao hao
2026-08-11 15:13:29
0
Shaibu Mohamed :
mh ushuzi m2pu nimatumizi mabaya ya muda
2026-08-11 14:52:57
0
Thabity Mziray :
soro
2026-08-11 14:18:52
0
Gody adventure :
vipngoz wa dini siyo wanachama wa upinzani na mwenyekiti wao ayuko jela
2026-08-11 17:56:38
0
To see more videos from user @uhondo.tv, please go to the Tikwm
homepage.