@denzel_trainer: Ukiona mtu amepata Ugonjwa huu wa Kiharusi (STROKE) na akawa amepata shida ya kuzungumza basi ni muhimu mgonjwa apatiwe Mtaalamu wa Mawasiliano( SPEECH THERAPIST), lakini vilevile hata kama Mgonjwa atakuwa anapatiwa Darasa na Mtaalamu wa Mawasiliano haina maana ya kwamba nyumbani asiendelee na tiba ya mazoezi ya mawasiliano na familia, na mazungumzo yake nyumbani yasiwe marefu sana, yanatakiwa kuwa anaongeleshwa maneno madogo madogo sana. Muepushieni Kelele za TV na RADIO, na muwe mnazungumza naye Uso kwa uso. MUNGU AKIJALIA KESHO NITAWAPA ELIMU ZAIDI JUU YA HILI NA HUYU MGONJWA.